JINSI YA KUSAFISHA LAPTOP
Hivi lini ilikuwa mwisho wa kusafisha laptop yako? je keys
za laptop yako zimeanza kugoma?laptop yako mpya imeanza kuonekana kama ya
zamani?
Kwa kukaa tu kwenye desk laptop yako huwa chafu,sikwambii
zinazozunguka katika siti za magari.Vumbi hujikusanya ndani ya laptop na sana
sana kwenye feni.Huilazimisha feni kuzunguka zaidi ambayo hatari yake ni
kuiruhusu kupata moto husababisha hata kufa .
Ni vizuri kuishi maisha ya raha na yenye afya na
yakipendezeshwa na laptop yako safiii…
Fuatilia njia hizi huenda ikatatua huo uchafu wa laptop
yako.
Tafuta dawa ya kusafishia-kwenye screen au kioo inabidi
utumie “screen
cleaner”.Kwa sehemu
nyingine
chukua bakuli tia sabuni kiasi,na
Isopropyl
alcohol.
Changanya mchanganyiko huo.
Kisha tumia
Chupa zile za kupulizia dawa ambazo zina mfuniko wa
kupulizia.
Zima compyuta yako na toa betri-usisafishe wakati unatumia.
Toa mouse,disc,cd’s,Usb,waya na chochote kilichochomekwa.
Chukua ile dawa pulizia,kuondoa uchafu.
Kama uchafu uko mwingi unaweza chukua kisu ukatoa keys kwa
uangalifu,waeza haribu connector, au kuumia wewe mwenye .
Weka bakuli la maji na sabuni kidogo,tia vile vikasha vya
keys ndani ya maji hayo kwa muda kubanduka yale mauchafu yalogandia.Ukisugua
tumia mkono au mswaki au brush ndogo ,tumia mswaki ambao hautumiki.
Tia bakuli nyingine maji ya uvguvugu na nusu kipimo cha Isopropyl alcohol.loweka
kitambaa kidogo kwenye huo mchanganyiko ,kamua maji yasichuruzikie kwenye
laptop.tumia kufutia ndani ya keyboards na uso wa laptop sio screen,ieleweke
hapoo.
Safisha katika mikunjo ya laptop tumia ule mchanganyiko wa
kupulizia mpaka isafishike vizuri.
Iache laptop kwenye hewa ipate kukauka.Usifunge mfuniko wa
laptop. Kama ulitoa keys tokea keyboards anza kuzifuta kwa kitambaa kikavu.
Anza kurudishia keys kwenye keyboards ukiwa una uhakika
mashine yako imekauka vizuri.
Tumia dawa maalum kupangusia screen.Pulizia kisha futa na
kitambaa kikavu.Hii iwe hatua ya mwisho katika usafi wako sababu isipate uchafu
tena,pindi usafishapo sehemu nyingine.
Usitumie sabuni za kawaida huweza haribu screen yako au
kupunguza performance yake,na hata uzuri wa mng’ao wa screen yako.
TIPS
Weka chakula mbali na laptop yako.Osha mikono kabla ya kutumia laptop yako .Kama utatoa keys,hakikisha unajua kurudishia,Tumia keyboard
nyingine kugelezea kurudishia keys au print copy yake ili upate picha kamili ya
keyboard ya laptop yako.Fanya hivyo kila unapotaka safisha laptop yako.
Pata kinywaji
ukipendacho baada ya usafi huo na furahia usafi huo kwani umekusaidia kupunguza
stress na umeinjoy piaUsiache kutembelea blog yetu ndani ya mtandao kujifunza mengi na mazuri zaidi.
safi!!
ReplyDeletenaipenda sana blogu yako na habarizako.
Ni blogu ya kipekee na habari za kipekee.
Hongera sana