CHUNUSI
Chunusi au Pimples ni aina ya
doa au madoa yanayosababishwa na mafuta ya ziada yaliyokuwa trapped katika
vinywelea.Nyingine ni Postules au Papules.Chunusi huweza tokea usoni,mabegani kifuani na
hata mgongoni.
Chunusi hutibika kwa aina ya dawa za kuondoa makovu ambazo
zimependekezwa na wataalamu,na hata kwa kununua za maduka ya dawa au urembo,kwa
mtazamo wa kujitibu.
SABABISHI:
Ndani ya vinywelea kuna Sebaceous gland,ambayo inazalisha “Sebum”.Pindi
layer ya nje ya ngozi inapoziba,seli ya ngozi zilokufa au kuisha, nyuma kushoto
hufanya kuganda kama gundi na huganda na sebum.
Hii husababisha vinywelea kujifunga,na sana sana pindi pale
ngozi inaposinyaa kama ya “kwapani”.Sebaceous glands huzalisha Sebum nyingi ambazo
hujenga nyuma juu ya pale palipoziba,na hii njia ya Sebum kuna kuwa na bacteria
wakiwemo kama Propionibacterium acnes,husababisha madhara na kuungua ambayo
huitwa chunusi.
TIBA ;
MADAWA YANAYOAGIZWA;
Kuna cream kwa ajili ya kutibu chunusi.
Dawa ya kawaida inayotibu na inayojulikana kwa chunusi ni Benzoyl Peroxide
na Salicylic
Acid na antibacterial kama Triclosan,zote hizo ni aina ya dawa hupatikana kwa
mfumo wa cream na gel na hutumika kwa kupakaa.Husaidia kutoa chunusi kwenye
ngozi kwa haraka na hulainisha ngozi pia.Huondoa bacteria kwa haraka.Kabla ya
kupakaa unatakiwa uoshe uso au sehemu husika kwa maji ya uvuguvugu na ukisha
ukaushe na taulo safi.
Cleanser huweza tumika kuoshea kwa nia ya kupakaa dawa.
Rosecea hii sio kwa ajili ya madhara yatokanayo na
bacteria.Madhara yalosababishwa na bacteria hutumika Tretinoin.
Kusafisha uso kuwa safi na kupakaa cream yatosha kuwa tiba nzuri ya chunusi japo
sio ya kudumu.
Aina ya kawaida na nzuri zaidi ni Benzoyl Peroxide,ina hatari ya ngozi
kidogo huweza sababisha allergy.
Kwa sasa Nicotinamide hupakaliwa kwa kipindi imeonyesha
kutibu zaidi kwa chunusi kuliko antibiotics kama Clindamycin.
Nicotinamide (VitaminB3)sio antibiotics na haina
madhara pia.Ina faida ya kupunguza Hyperpigmentation ambayo ni kisababishi cha chunusi.
DAWA(PRESCRIPTION MEDICATION).
Dawa nyingine hulazimika kuandikiwa na watalam kwa tiba ya
chunusi.Nayo ni Isotretinoin
ambayo ni Retinoid.
Historia yake ni antibiotics kama Tetracyclin na Erthromycin zimetajwa.Nazo zilikuwa
zinatibu zaidi kushinda Benzoyl Peroxide,Bacteria walikuwa sugu na
ikashindwa kupambana nao .Na antibiotics zinaonekana zina madhara zaidi kuliko
cream mfano wa kuumiza tumbo,huweza
kubadili rangi ya meno,zile antibiotics ziloelezwa na Dermatologist na wakashauri
ni Doxycycline na
Minocycline.Kwa
ajili ya kuondoa chunusi kwa mara moja.
Walishauri pia Accutane ambayo ilikuwa nzuri kwa kutibu chunusi
nayo. Hii Accutane
huweza sababisha madhara kama kutapika,kuharisha na matatizo ya uzazi kwa
wanawake.
TIBA YA
USAFI(HYGIENE).
Tumia njia hii mara kwa mara ;osha ngozi ilioathirika na
chunusi,tumia natural cleanser,husaidia kupunguza seli za ngozi zilokufa na
muingiliano wa bacteria ambazo ni sababu ya chunusi.
Japokuwa sio kama ndo inaweza kuondoa kabisa chunusi ila
hupunguza kasi ya chunusi kuendelea na kuenea na hata kuzuia pia.
Chunusi ni ngumu kutoka na huchukua muda mrefu.Madawa
yametengenezewa na madawa ambayo sio nzuuri kwa ngozi.Tumia njia hizi za asili
zifuatazo;
CHUMVI(SEA
SALT).
- · Chumvi ina detoxifying qualities hufanya kazi nzuri ya kukausha na kuondoa chunusi na madoa pia.
- · Chukua vijiko (3)vya chai vya chumvi weka ndani ya bakuli.
- · 1/2kikombe cha maji ya moto yalochemka sana,tia ndani ya bakuli uloweka chumvi.
- · Changanya na koroga pamoja tumia kijiti cha cotton buds .
- · Chukua upande wa kijiti hiko kina pamba kitakua kimelowa na maji yale .
- · Kisha weka kwenye chunusi au doa na shilkilia kwa dakika 10-20.
- · Unaweza fanya mara mbili kwa siku mpaka chunusi zikauke.
- · Unaweza tumia kitambaa kuwekea kwenye chunusi zilojikusanya sehemu moja nyingi.
BAKING SODA.
- · Osha uso tumia cleanser au sabuni ya uso.
- · Vijiko vya chai (8)vya baking soda weka kwenye chombo.
- · Tia maji kwenye chombo uloweka baking soda.
- · Koroga vizuri,iwe laini na uji uji yani isiwe nyepesi wala nzito sana iwe creamy.
- · Pakaa mchanganyiko huo katika chunusi .
- · Subiri kwa dakika 15 mpaka ikauke.
- · Osha na maji ya uvuguvugu.
- · Fanya hivi kwa wiki mara mbili(2)mpaka chunusi zipotee au kukauka.
- · Ikiwa uso utakuwa mkavu sana fanya mara moja(1)kwa wiki.ngozi ikianza kukauka zaidi ni bora upate ushauri wa daktari.
- Kumbuka kukauka kwa ngozi ni kawaida sababu chunusi husababishwa na mafuta yalozidi kwenye ngozi.
NJIA NYINGINE YA
KUONDOA CHUNUSI NYUMBANI KWAKO.
Barafu(ice)
1. Husaidia katika mzunguko wa damu katika sehemu
iloathirika,huondoa uchafu na mafuta yalolundikana kwenye ngozi.
2.
Weka barafu kwenye kitambaa kisha weka sehemu
ilo chunusi kwa dakika chache hivi kama unakanda.
Ndimu
1. Ina
Vitamin C,husaidia kukausha chunusi.
2.
Loweka kitambaa kwenye maji ya ndimu
ilokamuliwa,kisha pakaa,fanya hivyo kabla ya kulala waeza osha asubuhi au
kuosha baada ya nusu saa.Hakikisha unatumia ndimu ilo fresh ndio nzuri zaidi.
Asali
1. Hii
ina antibiotics na huzuia madhara ya bacteria,pakaa asali acha kwa nusu saa
kisha osha na maji ya uvuguvugu .
Dawa ya meno
1.
Wakati unapiga mswaki asubuhi na jioni pakaa
dawa hii pia kisha osha uso kwa maji ya uvuguvugu,na unaweza kulala nayo
ukaosha asubuhi .
Steam
1.
Weka maji kwenye bakuli maji ya uvuguvugu kisha
jifunuke na taulo kichwani ukiwa umeinamisha uso kwenye bakuli hili la maji kwa
dakika 10-20.
Kitunguu thoum(garlic)
1.
Hii ni antifungal,antiviral,antiseptic,na ina
sulfur pia.visage sugulia kwenye chunusi acha kwa dakika 5 kisha osha uso na maji ya
uvguvugu .Hata kula inasaidia kupurify damu,ila usile sana ina madhara tumboni.
Peppermint
1.
Maji ya majani yake ukiweza yapata ,yasugulie au
pakaa maji hayo kwa dakika (10).Osha uso kwa maji baridi.Hii ina antibacterial
na antiviral.
Tango
1.
Ni antioxidant,ina Potassium,Vitamin A,C,n
E.Loweka vipande vya tango kwenye maji kwa saa moja (1hr)virutubisho kama VitaminA, Potassium na Chlorophyll
vitaingia kwenye maji.Chuja maji na kunywa maji yake,au tumia kuoshea uso.
2.
Unaweza tumia kama mask.
3.
Saga tango moja kisha pakaa usoni kwa dakika(15)ikauke.kisha
osha kwa maji ya uvuguvugu.
Papai
1.
Ni antioxidant,Vitamin A,hulainisha ngozi tumia
kwa kupakaa kwenye chunusi.
habari njema kwa sisi wenye chunusi.
ReplyDeleteRekebisha dawa ya "mswaki" isomeke dawa ya meno
shukrani sana
Nimeelewa tayafanyia kaz
ReplyDelete