• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Monday, November 11, 2013

MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA.

11:20 PM // by Kalma // No comments

MAANDALIZI YA KUJIFUNGUA

Pole kwa uchovu wa safari ndefu. Kwa wiki (40)ulisubiria kufika hii siku.Ushaandikiwa siku ya kwenda.Mungu akipenda mwanao atakuja yuko njiani ,unakaribia kuacha kula kula vile ulokuwa ukivipenda kipindi hicho chote.Umeanza kusikia uchungu,na begi lako umepanga liko tayari. 
Tumia Castrol oil –husaidia kuleta uchungu,huweza kuharisha na kujisikia vibaya baya
  •         Kujua hospitali ni muhimu-na ulihudhuria kliniki utakuwa umeandikiwa ni hospitali gani,hii itakusaidia kujua tabia ya hospitali hiyo na masharti yake.
  •       Paki mabegi mawili lako na lingine la mtoto.
  •          Acha la mtoto kwenye gari au mkabidhi atakae kuangalia au partner wako,alijue liko wapi.
  •      Kadi ya hospitali na maternity ni muhimu.
  •          Gauni-huweza kutumia pindi utapochelewa kujifungua kufanyia mazoezi kwenye corido za  hospitalini.
  •      Viatu kama malapa au sandoes ya urahisi kuvaa na kuvua  yaani “open shoes”.
  •         Soksi –amini hili,miguu huweza pata baridi baada ya kujifungua.
  •         Night dress-inaweza kuwa t-shirt au diraa lilochokaa la zamani au la kushindia,huweza kuchafuka ,usinunue lipya kwa ajili ya labor hata hivyo ni muda mfupi tu.
  •          Massasge oil or Lotion-hutumika kukandia wakati wa labour,mafuta ya nazi pia mazuri.
  •          Lip balm-kwa ajili ya mdomoni kuzuia kukauka na kukatika kipindi cha baridi.
  •          Snacks na vinywaji- Glucose tablets,ni nzuri na kinywaji ukipendacho kisiwe kilevi ila cha moto kizuri zaidi kama chai n.k,husaidia kupoteza mawazo.
  •        Kitabu,magazine,kupoteza muda na kupumzika hata computer kama hospitali inaruhusu.
  •  Mto-maternity pillow kama wataruhusu ,kwa urahisi wa kupumzikia,kunyonyeshea.
  •        Simu na charger yake-kama smart phones uwe unaperuzi peruzi  kujua yanayoendelea kama habari na taarifa mbalimbali.
  •         Nguo ya kuondokea  nyumbani unaporuhusiwa  ni vizuri iwe kubwa isiwe ya kubana kama ternity au dira,hapa inaweza kuwa nguo mpya.
  •        Sidiria za kunyonyeshea mbili(2),au tatu(3).
  •         Pedi au vitambaa vya kuweka kwenye maziwa,huweza kutumia pamba ila hii haijashauriwa sanaa,siku hizi ziko pedi haswa kwa ajili ya kuweka kwenye maziwa,na kwa mwenye uwezo.
  •          Maternity pads za kutosha.

  •          Nguo au t-shirt yenye kufunguka mbele kwa ajili ya kunyonyeshea.
  •          Taulo,mswaki,kitana,dawa,sabuni  ya kuogea kwa  kutumia endapo utakaa hospitali kwa kusubiri uchunguzi n.k.
   Eye musks na earplugs kusaidia kwa kulala kwa wodi zenye kelele na usumbufu.
  • Ni vizuri na Yule aliyekusindikiza abebe snacks na vinywaji asihangaike kutafuta msosi  na sana nyakati za usiku,kuepusha kukuacha mwenyewe.
  • Kwa zile hospitali zenye kuruhusu partner kuingia labor room,waeza kubeba kamera kwa ajili ya picha za ukumbusho.

MAANDALIZI KWA MTOTO;

  •         Nguo za kulalia na vest
  •          Blanketi la mtoto.
  •        Nepi na chupi za mpira,kwa kawaida mtoto mchanga hujisaidia mara (12)kwa siku.
       Vitambaa vya kumfutia,baada ya kunyonya na akicheua .Soksi na bootie,usihangae bootie zipo zile aina ya uzi wa kufumia kama wa sweta.Nguo nzuri na haswaa mpya kwa ajili yakuondokea.
  Kofia,gloves za mikononi na Jacket au sweater.
  
Baby shoo au nguo za kumbebea.
Yashauriwa asali pia kwa ajili ya kumlambisha kidogo mtoto pindi atapozaliwa salama.
Kwa  mama mzazi ashauriwa kuoga maji ya moto kwa kipindi cha kukaribia kujifungua na baada ya kujifungua.






0 comments:

Post a Comment