KULAINISHA VIGANJA
Moja ya hasara ya mwanamke aliye hodari na kazi za nyumbani
ni viganja vya mikono kuwa vigumu au vikavu.Kama unafua na maji na
sabuni,kuosha vyombo,kusafisha nyumba,kubadili watoto nepi au
diapers,kupika n.k . usishangae kuwa na viganja
vigumu au vikavu.
Hakuna haja ya
kuogopa na toa wasiwasi hii ni aina ya kufanya mikono yako iwe laini na ya
kuvutia.Huna haja ya kwenda kwa spa’s wala kwa wataalamu.Baada ya kazi zako
fanya haya;
Kunywa maji kwa
wingi na tumia njia hizi zifuatazo;
Chukua container weka
chumvi kiasi.
Weka olive oil ndani ya container.
Weka sabuni ya maji
ya kuoshea mikono,tumia aina unayoipenda inaweza kuwa anti-bacterial au yoyote ya maji.Ni vizuri kutumia sabuni ya
maji sababu hautaosheka vizuri mkono sababu maji na mafuta hayachanganyiki.
Kausha mikono yako vizuri,kisha weka mchanganyiko huo kwenye
viganja vyako kisha sugua pole pole ,kiasi cha ½ kijiko cha chai.Sugua ndani na
nje ya viganja na ndani ya vidole na kucha.
Osha kwa maji ya uvuguvugu .
Kausha mikono kwa kutumia taulo kavu.
Pakaa lotion ya mikono .
Osha mikono na maji ya uvuguvugu na sabuni kuondoa grease na
bacteria.kisha kausha na taulo kavu.
Chukua sukari vijiko
viwili(2) vya chai na olive oil pia
vijiko viwili(2).
Pakaa mikononi kwa pamoja haraka .
Sugua mikono yote kwa pamoja ndani na nje kwa kutumia mchanganyiko huo.
Osha na maji ya uvuguvugu.
Tumia rose water pia nzuri .
Kisha pakaa lotion ya mkononi.
Waweza tumia pia
sunflower oil na hata mafuta ya nazi pia mazuri.
TIPS
Usifanye mara moja ukategemea matokeo ya kudumu au milele.Tumia baby oil au lotion kabla ya kulala.Tumia lotion zinazotengenezewa na mimea zaidi.Acha lotion kwa dakika kumi(10)kwenye viganja,ile layer ya
juu ya ngozi itanyonya lotion na italoki moisture ndani ya ngozi.Fanya hivi
mara mbili(2) kwa wiki.Vaa gloves au plastic wakati unafanya kazi kama kuosha
vyombo au gardening.Tumia Vaseline.
Kwa mikono mikavu zaidi unaweza kulala na gloves ukiwa
umepakaa lotion.
Usiache mikono kwenye maji baridi kwa muda
mrefu,huondoa mafuta na unyevu wa asili
mikononi.
Kuwa muangalifu na aina ya lotion utayotumia kuepusha athari
za allergies.
Hizi ni aina ya
lotion unaweza tumia kulainisha mikono :
The body hemp hand protector, Aron
moisture therapy intensive hand cream, L’Occitane shea Butter Hand Cream, Eurin
Intensive Repair Extra Enriched Hand Crème, Ahava Source Mineral Hand Cream,
Jaqua Raspberry Butter cream Frosting Hand Crème.
0 comments:
Post a Comment