• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, May 25, 2017

8 Rahisi za kuosha glass

12:55 AM // by Kalma // No comments

8 Rahisi za kuosha glass
Ni haraka na rahisi kuosha glass ambazo zinatoa harufu ya kunuka kama yai viza au zimapata ukungu mweupe ndani.Baada ya kuosha glaas,zinapata ukungu mweupe huonekana kama mawingu au hazijatakata.Kusafisha glass(za dongo au steel)hizi tips za kusafisha kuondoa uchafu huo na kuleta mng’ao .


Tips za kusafisha glass:

Loweka glass kwenye maji moto kabla ya kuziosha kwanza.hii husaidia kuondoa harufu mbaya na kuondoa madoa.Tia sabuni ya kuoshea vyombo kuondoa harufu ndani ya maji.Aina ya sabuni za ndimu au ukakasi ni nzuri zaidi kusafishia glass.


Acha glass ndani ya maji moto yenye sabuni kwa dakika 30-60 tumia maji kusuuza na tumia kisugulio cha plastic kusugulia ndani na nje ya glass.

 Unaweza tumia white vinegar husafisha glass kwa urahisi sana.Chemsha vinegar na maji au changanya kwenye maji moto.Sasa loweka glass chafu kwenye mchanganyiko wa vinegar ikiwa moto kwa 45 dakika.Tumia osheo la plastic kusugulia huondoa ukungu mweupe kwenye glass.Tumia sabuni ya vyombo kuoshea kasha suuza maji safi.Tumia kitambaa cha cotton kufutia na ziache zikauke.
Unaweza tumia vipande vya ndimu kusugulia glass.Osha glass kwa maji moto huku ukisugulia na vipande vya ndimu au limao.Ndimu au limao huondoa madoa na harufu .


Tia kijiko cha kula cha baking soda ndani ya maji moto na loweka glass kwa dakikia 30.Osaha glass za vinywaji tumia sabuni ya kuoshea vyombo suuza na maji safi.


Kama glass ina harufu ya chakula,tumia baking soda kuoshea au vipande vya ndimu au limao.Suuza na maji moto na futa kwa kitambaa cha cotton kikavu na kisafi.


Mara zote tumia kitambaa cha cotton kufutia glass baada ya kuziosha.Glass zinaonyesha sana yaani ziko wazi na huweka ukungu wa madoa ya vitone vya maji ambavyo vinaonekana vizuri.Mwaga maji kwenye glass mara tu baada ya kuosha na kusafisha .

Iache wazi glass kwa 10-15 dakika baada ya kuosha kuepusha kujenga ukungu hifadhi sehemu kavu.
Fuata njia hizi kung’arisha glass zako. 


Hizi tips zitakusaidia kuondoa harufu na uchafu kwenye glass zako.

Saturday, May 20, 2017

Njia ya kusafisha Lampshade

12:24 AM // by Kalma // No comments


Njia ya kusafisha Lampshade 


Nikiwa mkweli sipendi kusafisha vitu vya flani hivi sijui vinabore yaani(tedious things) kama mimea,vitu vya mapambo,na lampshades lakini mwisho wa siku ni vizuri kujua jinsi ya kuvisafisha,hata kama hausafishi mara kwa mara, kwasababu hivi vitu vinakusanya mavumbi na uchafu.


Njoo tuwe pamoja tujifunze jinsi ya kusafisha lampshade.

Mahitaji:
 Lint roller


 Kitambaa cha Microfiber


 Maji


Cha kwanza kabisa unachotakiwa ni kuondoa uchafu uliozunguka kwa lampshade.
Chukua kitambaa cha microfiber chenye maji yaani unyevu futia kwa kupitisha kufutia vumbi nje.


Kama uchafu upo ndani fanya kama hivyo pia.

Tumia kitambaa hicho hicho kusugua kama kuna madoa mfano ya wadudu au vidoti vya uchafu.


Mpaka hapo kitambaa kitakua kimejaa vumbi kisafishe au kikunje sehemu safi utasafishia tena ndani na nje.(na hii wengi baadhi husahau)


Unaendelea kutumia kitambaa chako cha microfiber kikiwa safi kwa nje na utafuta na bulb yenyewe.
Hutakiwi kutumia dawa au king’arishi kusafisha lampshade uchafu wake mkubwa ni vumbi.

 Ndio haswaa vumbi hugandia sana kwenye au juu ya bulb lakini usafi wake nao ni rahisi


kusafisha bulb
 Ilaze au izungushie microfiber kwenye bulb kiache kwa 3-5 dakika .Baada ya muda huo kitambaa kitakua kimefyonza uchafu na kIsha futa taratibu.Hicho kitambaa kitatoa uchafu bila ya kusugua na kuepusha hatari ya kuvunja bulb.

 Kusafisha lampshade huenda ikawa sio fun angalau lakini umejua jinsi ya kusafisha kwa njia rahisi!

   

Thursday, May 18, 2017

Kwanini Sakamia ikusafishie carpet?

4:27 AM // by Kalma // No comments

Unafikiria kusafishiwa carpet?


Kinachofunika sakafu nyingi majumbani na ofisini na ukajisikia raha kwa kulikanyaga kwake,ni jukumu lako kulitunza vyema carpet lako.Kulitunza carpet lako ni kulisafisha mara kwa mara liwe safi.
 
Kiukweli,uchafu kwenye carpet ndio unaoruhusu vijidudu na mazalio ya pests ambayo ni hatarishi  kwa afya yako na familia kwa ujumla.Kulisafisha carpet mwenyewe huongeza hatari ya kuliharibu carpet ni pale ambapo huna ujuzi zaidi wa kusafisha aina za uchafu na matumizi ya vifaa maalumu kwa carpet lako.


 Kwa matokeo mazuri zaidi yaani excellent,inashauriwa kupata kampuni yenye utaalamu wa kusafisha carpet.


Kuleta kusafishiwa carpet ni rahisi kutumia utaalam wetu dhidi ya carpet lako.Kuna kampuni nyingi zinatoa huduma hii lakini sakamia inashika namba.Na hizi ni sababu chache kwanini utuchague kukusafishia carpet lako.

Techniques za mazingira rafiki


Pamoja na dunia kuwa kijani,kikubwa tunachotaka kuwa na mchango mkubwa duniani.Kutokana na hilo,tunatumia njia rafiki ya kukusafishia carpet lako.Njia tunayotumia ni sahihi kwa fibres kwenye carpet zimesalimika  na sumu.

 

Kwahiyo,utakua na mapumziko ya uhakika baada ya kusafishiwa carpet na sakamia,hakuna atakae hisi allergies au maambukizi yatayosababishwa na madhara ya dawa.Kiufupi,hatusafishi carpet lako tu,vile vile tunachangia kutunza mazingira yetu.

Kuvalisha cover kwa carpet


Carpet sehemu za watu wengi kama majengo ya biashara na ofisi za serikali matumizi yake ni makubwa zaidi kwasababu ya wingi wa watu ndani ya hizi sehemu.Hizi carpet zinachafuka haraka,zinahitaji kusafishwa mara kwa mara.

Tatizo hata kwa utaalam wa hali ya juu,kurudia kusafisha carpet inazidisha kuharibika kwa fibers za kwenye carpet.Tofauti na kampuni nyingine za kusafisha carpet,tunakuoffer namna ya kuyadhibiti matatizo na kulitunza carpet,utachagua kuwa na special cover kwa kufunikia carpet lako inayosaidia kutochafuka haraka.Kwa kufanya hivyo,inachukua muda mrefu kidogo kuhitaji usafi wa carpet tena.

Budget 


Carpets ni ghali kiukweli.Ili kulitunza angalau lidumu kwa muda mrefu yaani (decade).Ukifikiria athari ya kuweka carpet jingine baada ya mwaka kwasababu umeliharibu,unahitaji huduma zetu.Kwa kutuchagua sisi sakamia,carpet lako linakua safi kitaalamu kwa wataalamu wanaojua kindaki ndaki faida na hasara ya kung’ara kuwa mfano wa jipya.

Zaidi,tutakushauri jinsi ya kulitunza carpet lako baada ya kusafisha na  hii itakusaidia kusave hela kwa muda mrefu.

Tunajali muda


Wanasema muda ni hela.Usafi wa carpet ni zoezi pevu linalohitaji muda.Kutuita sakamia wakusafishie itakusevia muda na mahangaiko ya kutoa uchafu(kuhangaika kutoa madoa na mafuta yalogandia)wakati ungetumia muda wako huo kuzalisha zaidi na kufanya yenye manufaa katika jamii.


Kwa kumalizia,tunajali na kuthamini wateja wetu, na kila leo tunafikiri njia mpya tofauti kuwahudumia wateja.Tuchague sakamia kama wasafishaji wako wa carpet na tutakuacha ni mwenye kuridhika wewe na kwa carpet lako pia.


Wednesday, May 17, 2017

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwa friji

1:36 AM // by Kalma // No comments

Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwa friji
 Kuweka friji kuwa fresh
Unukaji wa friji uko kinamna nyingi.Huweza sababishwa kwa kumagika kwa maziwa na hata mayai yaliyosahauliwa kwa muda mrefu.Ushawahi kusahau viazi katika kibebeo cha mboga mboga?Hua inaleta harufu mbaya kuliko unavyofikiria.Madoa mengine yanang’ang’ania kuliko mengine,madoa mengine ni ya asili,lakini sio wazo zuri kuyaacha kwasababu yanaweza kuenea na kuharibu kila sehemu ya friji na yakasababisha uharibifu hadi kwa miundo mbinu ikawa tabu kusafisha kwake.
Lakini subira ndogo tu na matunzo yanazaa mafanikio ya utunzaji wa friji lako.
Njia ni hizi zifuatazo:
Toa kila kitu nje
Hata kama umegundua sehemu yenye uchafu,unatakiwa utoe vitu vyote kwenye friji na friza.Kama una friji mbili unaweza hamishia vitu huko kwa muda.Kama uchafu ni sababu ya kuzima friji,usitoe vitu ukiwa hauko tayari kusafisha kwasababu friji linahifadhi kwa muda wa saa 4,kama itadumu imefungwa.
Osha kwa mkono bins na shelves





Toa shelves ,bins,droo,trei za barafu,na chochote kinachotoka na uvioshe kwenye sink tumia sabuni na maji moto.Kwa friji lenye harufu,changanya kijiko cha kula kimoja(1)cha chlorine bleach kwenye galoni la maji na tumia mchanganyiko huo kufutia kwenye shelfu chini na bins pia;suuza kwa maji safi na kausha kwa kitambaa safi.
Manukato ndani ya friji


Sasa utakua tayari kuosha ndani ya friji.Tumia mchanganyiko wa kikombe kimoja(1)cha baking soda kwa gallon la maji.Futa ndani ,chini kwa kutumia sponji ulowekee mchanganyiko huo.Kwa vifungashio vya chakula pitisha sponji juu kisha futa kwa kitambaa safi.Usitumie kifaa kigumu kwa kusugulia friji huweza kuchubua friji lako.
Kukausha

Hapa panataka subra kidogo.Kwa matokeo mazuri,unatakiwa uzime friji,acha milango wazi,uliache kwa siku nzima.Kama litaendelea kutoa harufu tumia mchanganyiko wa baking soda kufutia tena na uliache kwa siku nzima tena.Hapa kwa friji lenye harufu kali na haikufanikiwa kuisha .
Tip
kuileta harufu nzuri kwa friji,weka pamba ambazo zimelowekwa na vanilla ndani ya friji na friza halafu funga kwa saa kadhaa kabla ya kurudishia vitu.
Kusafisha evaporator
Kama bado kuna harufu na haijaisha,nafasi kubwa ya harufu itakua inatokea kwa evaporator coil,ambayo hutoa hewa ya baridi kwenye friji na friza.Coil,ikiambatana na feni husambaza hewa,zimewekwa ukutani  wa nyuma ya friji au friza.
Anza kwa kutoa screw ambazo zinashikilia kifungashio.Chomoa kwenye umeme na kitengeneza barafu. Toa na osha panel.Tumia chupa ya kipulizo yenye maji moto ya sabuni kwenye coil,zuia maji machafu yamwagikayo na kitambaa;rudia na maji safi kwa kusuuza.Iache coil ikauke kabisa kabla ya kuifunga na panel.
Kazi hii ni rahisi,hakikisha unaweka friji au friza sehemu ambayo unaweza kusafisha kwa nyuma.Tumia kitabu cha maelezo yaani manual kwa maelezo zaidi.
Jua kama una friji jipaya yaani ya kisasa yenye dual evaporator ,itakua ina coil mbili,moja ni kwa friza na nyingine kwa friji.Kama uchafu ni sehemu ya chakula yaani friji utasafisha coil husika.

Saturday, May 6, 2017

Ng’arisha chumba chako

7:47 AM // by Kalma // No comments

Ng’arisha chumba chako
Kitanda, Furniture,mapambo,taa,pambo za ukutani & vioo   
       


 Unajua kwamba ni mapumziko tosha muonekano wa chumba chako kwa mabadiliko madogo tu?Huitaji furniture mpya  au kupaka rangi tena,japokuwa kupakaa rangi mpya nayo ni vizuri.Unaweza kubadili uonekano wa chumba chako kwa kukipangilia furniture hizo hizo ulizokuwa nazo,bila ya gharama yoyote.Kama hii haitoshi badili duvet cover,kwa kitanda chako au kitanda chako kihamishie upande mwingine.
Rangi za shuka

Kwa muda mrefu kidogo napendelea mashuka ya rangi zilizokooza ,familia yangu wanapenda pia tuliona tunaendeana . Kwa sasa nimebadili natumia rangi zilizopoa yaani cool colours au rangi za kizungu kwa jina lingine.Maua machache yenye rangi ya njano na zambarau,mito mingi mingi aina tofauti unachanganya rangi ya foronya.Hua najisikia mapumziko makuu niingiapo chumbani kwangu.
kioo
Hata ukiwa na chumba kidogo,unaweza kuongeza kioo upande mmoja wa kitandani  vile virefu designed kizuri kitu amaizing,utahisi chumba kikubwa kinawaka na kisafi.Vioo huvutia na kuongeza mwanga kwa chumba kidogo kinafaidi mwanga mwingi na ukubwa umeongezeka.
Maua
Maua yawe ya ukweli au ya mapambo hubadili muonekano wa chumba.Huongeza uhalisia na uzuri kila mahala.Unaliweka sehemu nzuri inayokupendeza basi huvutia kwa kuliangalia kwake na kuchanua kwake,huleta furaha litoapo harufu.Unalipamba vizuuri inaweza ikawa kwenye kona,au juu ya meza ndogo ya pembeni kitandani n.k.
Kiti 
kizuri chenye rangi nzuri inayoendana na mapambo ya ndani ya chumba .Utajishangaa saa zote upo chumbani kwako maana kinakupa faraja na kukupumzisha.Kiweke kwenye kona ambayo unaweza kusoma vitabu huku unaangalia dirisha,au upande iliko Tv,kama chumba cha ghorofa unaangalia view ya nje ukipata hali ya hewa fresh na salama kwa afya yako.
Yote hayo yatakupumzisha chumbani kwako kwa gharama nafuu .Najua unaweza kufanya vizuri zaidi .

ENJOY !