Jinsi ya kuondoa harufu mbaya kwa friji
Kuweka friji kuwa fresh
Unukaji wa friji uko kinamna nyingi.Huweza sababishwa kwa
kumagika kwa maziwa na hata mayai yaliyosahauliwa kwa muda mrefu.Ushawahi
kusahau viazi katika kibebeo cha mboga mboga?Hua inaleta harufu mbaya kuliko
unavyofikiria.Madoa mengine yanang’ang’ania kuliko mengine,madoa mengine ni ya asili,lakini
sio wazo zuri kuyaacha kwasababu yanaweza kuenea na kuharibu kila sehemu ya
friji na yakasababisha uharibifu hadi kwa miundo mbinu ikawa tabu kusafisha
kwake.
Lakini subira ndogo tu na matunzo yanazaa mafanikio ya
utunzaji wa friji lako.
Njia ni hizi zifuatazo:
Njia ni hizi zifuatazo:
Toa kila kitu nje
Hata kama umegundua sehemu yenye uchafu,unatakiwa utoe vitu
vyote kwenye friji na friza.Kama una friji mbili unaweza hamishia vitu huko kwa
muda.Kama uchafu ni sababu ya kuzima friji,usitoe vitu ukiwa hauko tayari
kusafisha kwasababu friji linahifadhi kwa muda wa saa 4,kama itadumu imefungwa.
Osha kwa mkono bins na shelves
Toa shelves ,bins,droo,trei za barafu,na chochote
kinachotoka na uvioshe kwenye sink tumia sabuni na maji moto.Kwa friji lenye
harufu,changanya kijiko cha kula kimoja(1)cha chlorine bleach kwenye galoni la
maji na tumia mchanganyiko huo kufutia kwenye shelfu chini na bins pia;suuza kwa
maji safi na kausha kwa kitambaa safi.
Manukato ndani ya friji
Sasa utakua tayari kuosha ndani ya friji.Tumia mchanganyiko
wa kikombe kimoja(1)cha baking soda kwa gallon la maji.Futa ndani ,chini kwa
kutumia sponji ulowekee mchanganyiko huo.Kwa vifungashio vya chakula pitisha
sponji juu kisha futa kwa kitambaa safi.Usitumie kifaa kigumu kwa kusugulia
friji huweza kuchubua friji lako.
Kukausha
Hapa panataka subra kidogo.Kwa matokeo mazuri,unatakiwa
uzime friji,acha milango wazi,uliache kwa siku nzima.Kama litaendelea kutoa
harufu tumia mchanganyiko wa baking soda kufutia tena na uliache kwa siku nzima
tena.Hapa kwa friji lenye harufu kali na haikufanikiwa kuisha .
Tip:
kuileta harufu nzuri kwa friji,weka pamba ambazo
zimelowekwa na vanilla ndani ya friji na friza halafu funga kwa saa kadhaa
kabla ya kurudishia vitu.
Kusafisha evaporator
Kama bado kuna harufu na haijaisha,nafasi kubwa ya harufu
itakua inatokea kwa evaporator coil,ambayo hutoa hewa ya baridi kwenye friji na
friza.Coil,ikiambatana na feni husambaza hewa,zimewekwa ukutani wa nyuma ya friji au friza.
Anza kwa kutoa screw ambazo zinashikilia kifungashio.Chomoa
kwenye umeme na kitengeneza barafu. Toa na osha panel.Tumia chupa ya kipulizo
yenye maji moto ya sabuni kwenye coil,zuia maji machafu yamwagikayo na
kitambaa;rudia na maji safi kwa kusuuza.Iache coil ikauke kabisa kabla ya
kuifunga na panel.
Kazi hii ni rahisi,hakikisha unaweka friji au friza sehemu
ambayo unaweza kusafisha kwa nyuma.Tumia kitabu cha maelezo yaani manual kwa
maelezo zaidi.
Jua kama una friji jipaya yaani ya kisasa yenye dual
evaporator ,itakua ina coil mbili,moja ni kwa friza na nyingine kwa friji.Kama
uchafu ni sehemu ya chakula yaani friji utasafisha coil husika.
0 comments:
Post a Comment