Njia 5 za kutakatisha nguo nyeupe bila bleach
Achilia mbali kusugua kuondoa madoa,baking soda husaidia
kutoa madoa na kuifanya nguo kuwa laini
yaani soft pindi ufuapo.Hakikisha unasuuza vizuri na sabuni utumiayo na
punguza matumizi ya bleach kuanzia sasa.
Jinsi ya kutakatisha nguo nyeupe bila bleach
Nguo nyeupe hushika madoa kirahisi sana hata ukiwa makini,au
hata baada ya kuvaliwa huanza kuleta rangi ya njano flani hivi.
Kuifanya ing’ae siku zote kwa weupe wake, mara zote hutumika
dawa zipatikanazo madukani kwa siku hizi,ambazo nyingi kati ya hayo madawa yana
bleach na kuaminika ndio suluhisho bora zaidi kwa kung’arisha nguo nyeupe na
nyinginezo.
Kiukweli hizi products zinafanya kazi vizuri yaani zinang’arisha
vizuri,na huenda ikawa njia rahisi ya kupata mng’ao wa weupe katika nguo.Lakini
madawa yaliyomo kwa dawa hizo sio nzuri kwa afya kabisa,ni hatarishi hata kwa
mazingira yetu.
Kujilinda na vihatarishi kwa kutumia dawa za bleach na dawa
zenye bleach,article ya leo tunataka kwa pamoja kushare njia za kufua na kung’arisha
nguo zako kwenye mazingira rafiki
zaidi,kwa kutumia vitu asili ambavyo utavihifadhi nyumbani kwako kutoa madoa na kung’arisha nguo
zako na kurudisha weupe wake wa upya.
White vinegar
Potezea matumizi ya kutumia dawa za kuondoa madoa na uchafu
sugu,white vinegar ni rahisi kuondoa madoa hayo na husaidia nguo kuwa soft
kiasili badala ya kulainishwa na madawa mbalimbali.
Tumia ½ -1 kikombe
cha distilled white vinegar kufulia kawaida kila mara, na hata ndani ya washing
mashine,na tumia mashine kawaida utumiavyo.
Kama nguo zako zina
madoa au uchafu shingoni,makwapani, mifukoni au sehemu yoyote,sugua kwa kutumia
white vinegar maeneo hayo na iache kwa saa nzima kabla ya kufua .
Baking soda
Baking soda hii ni nyongeza ambayo inapatikana
kirahisi,inapenya kwenye kina cha madoa katika nguo,huondoa madoa na kulainisha
pia.
Weka ½ kikombe cha
baking soda wakati wa kufua tumia kama dawa ya madoa na ufue kawaida. Kumbuka mara
zote kutofautisha na usichanganye nguo nyeupe na za rangi. Kwa madoa
sugu,changanya baking soda na maji ya ndimu kidogo moja kwa moja kwenye yale
madoa.
Hydrogen peroxide
Hydrogen peroxide ni dawa nzuri sana kwa kuleta mng’ao kwa
nguo nyeupe kwasababu haina bleach.
weka ½ kikombe cha
3% ya hydrogen peroxide pindi ufuapo.Tumia moja kwa moja kwenye madoa pia.
Maji ya ndimu
Maji ya ndimu nayo ni ya asili yanayotakatisha na kung’arisha
kwenye kina cha fiber,huondoa madoa na uchafu na kuiacha nguo safi na manukato
mazuri na nyeupe.
Tia maji kwa
beseni na vipande vya ndimu,chemsha,kisha loweka nguo zako kwa muda wa saa nzima
kabla ya kufua.
Njia nyingine
mchanganyiko wa maji na sabuni,kijiko cha chakula cha chumvi,na maji ya ndimu
mbili.Loweka nguo kwa mchanganyiko huo,suuza na anika juani.
Maziwa
Hii hata sisi tumestaajabu,ni mshangao!unaweza tumia kung’arishia
nguo zako na upya wa weupe kupatikana. Ushauri wa matumizi ni nguo za cotton
haswaa na zile delicate fabrics.
Matumizi?
Tia nguo kwa beseni
lenye maziwa na loweke kwa saa kadhaa,kabla ya kusuuza kawaida.
Tips
Nguo nyeupe inahitaji matunzo ya ziada ili iwe kwenye hali
ya mng’ao na safi yenye rangi ya kuvutia.
Kama nguo nyeupe ndizo upendazo tuwe pamoja kwenye hizi tips:
Epuka utumiaji wa
bleach kwa nguo aina ya polyester au cotton-polyester, mchanganyiko wa bleach na polyster unaweza kusababisha polyster
ikabadilika ikawa njano.
Umakini zaidi kwa
maji utumiayo pindi ufuapo,kama sio masafi husababisha nguo kuwa njano.
Pindi ufuapo nguo
nyeupe tia borax iliyochanganywa kwenye maji kulainisha nguo.Borax haileti
madoa kwenye nguo.
Jihadhari madoa
doa kwenye nguo nyeupe,hakikisha hutumii perfume,deodorant,au kisababishi
chochote cha madoa.Hizi ni sababu ya kufanya nguo kuwa njano.
Mara zote anika nguo nyeupe juani,kwasababu UV
rays husaidia kung’arisha zaidi.
0 comments:
Post a Comment