8 Rahisi za kuosha glass
Ni haraka na rahisi kuosha glass ambazo zinatoa harufu ya
kunuka kama yai viza au zimapata ukungu mweupe ndani.Baada ya kuosha
glaas,zinapata ukungu mweupe huonekana kama mawingu au hazijatakata.Kusafisha
glass(za dongo au steel)hizi tips za kusafisha kuondoa uchafu huo na kuleta
mng’ao .
Tips za kusafisha glass:
Loweka glass kwenye maji moto kabla ya kuziosha kwanza.hii
husaidia kuondoa harufu mbaya na kuondoa madoa.Tia sabuni ya kuoshea vyombo
kuondoa harufu ndani ya maji.Aina ya sabuni za ndimu au ukakasi ni nzuri zaidi
kusafishia glass.
Acha glass ndani ya maji moto yenye sabuni kwa dakika 30-60
tumia maji kusuuza na tumia kisugulio cha plastic kusugulia ndani na nje ya
glass.
Unaweza tumia white vinegar husafisha glass kwa urahisi sana.Chemsha vinegar na maji au changanya kwenye maji moto.Sasa loweka glass chafu kwenye mchanganyiko wa vinegar ikiwa moto kwa 45 dakika.Tumia osheo la plastic kusugulia huondoa ukungu mweupe kwenye glass.Tumia sabuni ya vyombo kuoshea kasha suuza maji safi.Tumia kitambaa cha cotton kufutia na ziache zikauke.
Unaweza tumia vipande vya ndimu kusugulia glass.Osha glass
kwa maji moto huku ukisugulia na vipande vya ndimu au limao.Ndimu au limao
huondoa madoa na harufu .
Tia kijiko cha kula cha baking soda ndani ya maji moto na
loweka glass kwa dakikia 30.Osaha glass za vinywaji tumia sabuni ya kuoshea
vyombo suuza na maji safi.
Kama glass ina harufu ya chakula,tumia baking soda kuoshea
au vipande vya ndimu au limao.Suuza na maji moto na futa kwa kitambaa cha
cotton kikavu na kisafi.
Mara zote tumia kitambaa cha cotton kufutia glass baada ya
kuziosha.Glass zinaonyesha sana yaani ziko wazi na huweka ukungu wa madoa ya
vitone vya maji ambavyo vinaonekana vizuri.Mwaga maji kwenye glass mara tu
baada ya kuosha na kusafisha .
Iache wazi glass kwa 10-15 dakika baada ya kuosha kuepusha
kujenga ukungu hifadhi sehemu kavu.
Fuata njia hizi kung’arisha glass zako.
Hizi tips zitakusaidia kuondoa harufu na uchafu kwenye glass
zako.
0 comments:
Post a Comment