Shampoo hutumika vizuri kama sabuni
ya mikono,na ni rahisi kuliko sabuni ya kununua.Tia robo shampoo kwenye
kifungashio changanya na maji,tikisa ichanganyike vizuri.
Shaving
Cream
Punguza kununua shaving cream katika
list ya matumizi yako.Tumia shampoo na inafanya vizuri,na haiachi uchafu wa madoa
ya kutu katika bafuni au tub yako.
Tip:
Changanya shampoo na conditioner pamoja au tumia zote kwa pamoja huifanya ngozi
kuwa laini na nyororo.
Sabuni ya
kuogea
Tunzafedha na punguza namba za chupa
za sabuni ya kuogea bafuni kwako kwa kutumia shampoo mwilini kwako.Hulainisha
ngozi na hukuacha na manukato mazuri mwilini.
Tia shampoo kwenye maji ya kuogea
kupata mapovu wakati wa kuoga
Changanya chumvi au sukari kwa
shampoo tumia kama scrub ya mwilini
Kufulia nguo
Sahau kununua sabuni ya
kufulia.Nyunyiza shampoo kwenye beseni au sink la kufulia lenye maji,inatumika
kwa nguo za ndani,sweta,na aina ya nguo za kawaida.Fua kwa mkono.
Kuondoa madoa
Nyunyizia shampoo kwenye doa la
nguo.Haswa aina ya mafuta,na madoa ya damu.Tia shampoo kwenye doa iache kwa muda
kidogo,fikicha,suuza vizuri.Rudia ikilazimika.
Madoa ya
carpet
Huondoa madoa kwenye carpet
,sofa,kochi.Tia shampoo ni rhisi sugua na kitambaa au sponji mpaka pawe safi.
Muhimu: Ondoa madoa kwenye carpet na
sofa au kochi mara tu lichafukapo.
Tip:
ondoa wasiwasi wa kUvujia rangi kwa kujaribu eneo lingine kwanza.
Jikoni
Tumia shampoo kuondoa mafuta jikoni
yaliyogandia kwenye counters,ukutani,stove,na vifaa vilivyopo.Tia shampoo
kidogo kwenye kitambaa cha unyevu nyevu.Safisha sehemu chafu,iache kwa muda
kidogo.Suuza mpaka pawe safi.
Tip: Changanya shampoo na baking soda huondoa uchafu haraka zaidi.
Sakafu(Floor)
Changanya shampoo kidogo na maji ya uvuguvugu .Hung’arisha
vizuri tiles,aina ya tarazo,na harufu nzuri.
Bafuni(Bathroom)
Shampoo imetengenezwa kukata au
kusafisha mafuta kirahisi na kukuza nywele,inafanya vizuri katika kufyonza
mafuta kama sabuni.Tumia kusafishia tub au shower kwa kutumia kitambaa,utapunguza
muda wa kusugua.Iache kwa muda kidogo,suuza na safisha vizuri.Utastaajabu
uchafu wote umesafishika na pameng’aa.
Spray ya nywele imegandia kwenye
ukuta wa bafuni kwako?shampoo pia huondoa uchafu huo.
Mapovu
Watengenezee watoto mapovu ya
shampoo changanya na maji.Inakua sawa kama zile za kununua na gharama ndogo.
ENJOY NA SHARE!
0 comments:
Post a Comment