Ng’arisha chumba chako
Kitanda, Furniture,mapambo,taa,pambo za ukutani & vioo
Unajua kwamba ni mapumziko tosha muonekano wa chumba chako kwa mabadiliko madogo tu?Huitaji furniture mpya au kupaka rangi tena,japokuwa kupakaa rangi mpya nayo ni vizuri.Unaweza kubadili uonekano wa chumba chako kwa kukipangilia furniture hizo hizo ulizokuwa nazo,bila ya gharama yoyote.Kama hii haitoshi badili duvet cover,kwa kitanda chako au kitanda chako kihamishie upande mwingine.
Rangi za shuka
Kwa muda mrefu kidogo napendelea mashuka ya rangi
zilizokooza ,familia yangu wanapenda pia tuliona tunaendeana . Kwa sasa nimebadili
natumia rangi zilizopoa yaani cool colours au rangi za kizungu kwa jina
lingine.Maua machache yenye rangi ya njano na zambarau,mito mingi mingi aina
tofauti unachanganya rangi ya foronya.Hua najisikia mapumziko makuu niingiapo
chumbani kwangu.
kioo
Hata ukiwa na chumba kidogo,unaweza kuongeza kioo upande
mmoja wa kitandani vile virefu designed
kizuri kitu amaizing,utahisi chumba kikubwa kinawaka na kisafi.Vioo huvutia na
kuongeza mwanga kwa chumba kidogo kinafaidi mwanga mwingi na ukubwa
umeongezeka.
Maua
Maua yawe ya ukweli au ya mapambo hubadili muonekano wa
chumba.Huongeza uhalisia na uzuri kila mahala.Unaliweka sehemu nzuri
inayokupendeza basi huvutia kwa kuliangalia kwake na kuchanua kwake,huleta
furaha litoapo harufu.Unalipamba vizuuri inaweza ikawa kwenye kona,au juu ya
meza ndogo ya pembeni kitandani n.k.
Kiti
kizuri chenye rangi nzuri inayoendana na mapambo ya
ndani ya chumba .Utajishangaa saa zote upo chumbani kwako maana kinakupa faraja
na kukupumzisha.Kiweke kwenye kona ambayo unaweza kusoma vitabu huku unaangalia
dirisha,au upande iliko Tv,kama chumba cha ghorofa unaangalia view ya nje
ukipata hali ya hewa fresh na salama kwa afya yako.
Yote hayo yatakupumzisha chumbani kwako kwa gharama nafuu
.Najua unaweza kufanya vizuri zaidi .
ENJOY !
0 comments:
Post a Comment