• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Saturday, May 20, 2017

Njia ya kusafisha Lampshade

12:24 AM // by Kalma // No comments


Njia ya kusafisha Lampshade 


Nikiwa mkweli sipendi kusafisha vitu vya flani hivi sijui vinabore yaani(tedious things) kama mimea,vitu vya mapambo,na lampshades lakini mwisho wa siku ni vizuri kujua jinsi ya kuvisafisha,hata kama hausafishi mara kwa mara, kwasababu hivi vitu vinakusanya mavumbi na uchafu.


Njoo tuwe pamoja tujifunze jinsi ya kusafisha lampshade.

Mahitaji:
 Lint roller


 Kitambaa cha Microfiber


 Maji


Cha kwanza kabisa unachotakiwa ni kuondoa uchafu uliozunguka kwa lampshade.
Chukua kitambaa cha microfiber chenye maji yaani unyevu futia kwa kupitisha kufutia vumbi nje.


Kama uchafu upo ndani fanya kama hivyo pia.

Tumia kitambaa hicho hicho kusugua kama kuna madoa mfano ya wadudu au vidoti vya uchafu.


Mpaka hapo kitambaa kitakua kimejaa vumbi kisafishe au kikunje sehemu safi utasafishia tena ndani na nje.(na hii wengi baadhi husahau)


Unaendelea kutumia kitambaa chako cha microfiber kikiwa safi kwa nje na utafuta na bulb yenyewe.
Hutakiwi kutumia dawa au king’arishi kusafisha lampshade uchafu wake mkubwa ni vumbi.

 Ndio haswaa vumbi hugandia sana kwenye au juu ya bulb lakini usafi wake nao ni rahisi


kusafisha bulb
 Ilaze au izungushie microfiber kwenye bulb kiache kwa 3-5 dakika .Baada ya muda huo kitambaa kitakua kimefyonza uchafu na kIsha futa taratibu.Hicho kitambaa kitatoa uchafu bila ya kusugua na kuepusha hatari ya kuvunja bulb.

 Kusafisha lampshade huenda ikawa sio fun angalau lakini umejua jinsi ya kusafisha kwa njia rahisi!

   

0 comments:

Post a Comment