Mmea wa Aloe
Matumizi na faida zake
Mmea wa Aloe una matumizi na faida kibao,na mmea aloe kiukweli ni kitu ambacho napenda kiwepo nyumbani,na haswa kipindi cha jua au kiangazi.
Ni cha ajabu mmea huu kwa kulainisha ngozi baada ya kupigwa na jua kali ndani ya siku yako,hata kama halijakuunguza (sunburnt),na vile vile hutumika kuondoa scrapes na kuungua kidogo.
Mara zingine sikumbuki niliweka wapi chupa la mmea wa aloe najikuta nakimbizana kuitafuta huku na huku na hata hujisikia vizuri pale watu wanapouzungumzia mmea huu na hufarijika nikisikia mmoja wao anao nyumbani kwake.
Napendelea zaidi kuifanya mimea iwe hai kila leo,na sina mkono mzuri wa kustawisha mmea,lakini mmea wa Aloe ni rahisi kuufanya uwe hai kila siku.
Unaweza kuuotesha ndani bila hata kuitaji jua wala maji.Na ukaishi kwa miaka kwa miaka,na ukawa mkubwa vizuri tu.
Faida za kuwa na mmea Aloe nyumbani?
Muda wowote nikiuhitaji nachokifanya ni kukata kipande ambacho ni fresh ni kizuri,halafu mara moja hujifunga na kumea tena, wala huhitaji kuwa na wasiwasi kwa kuota kwake.
Aloe gel inapatikana hapo clear,ni jelly ambayo inapatikana ndani ya katikati ya mmea huu mwa jani lake.
Mmea huu unazalisha material inayoitwa aloe latex inapatikana chini ya ngozi ya mmea na ni rangi ya njano.
Hutumika kwa kupunguza maumivu ya kuungua kwa jua na hata kuungua kwa aina yoyote ile,aloe gel pia hutumika kuondoa madoa au kovu,psoriasis,na hulainisha ngozi pia.
Kwa matumizi ya urembo hauna mwisho.
Gel ya mmea huu unaweza sugulia kwenye ngozi ya kichwa kwa kukuza na kuotesha nywele,na kupakaa kwenye kiganja na kusugulia kwenye nywele hulainisha nywele na kuondoa ukavu wa nywele.
Nimejaribu kufikiria kuja kutengeneza shower gel na lotion.
Kama una jua zaidi faida za mmea huu nijuze!
0 comments:
Post a Comment