Licha ya nguvu nyingi ya usafi wa carpet lako,hatimaye hua
ni muathirika wa madoa,kumwagikiwa,ajali za hapa na pale,na vile vilivyobebwa
na viatu.Kujua utaalam wa kulifanya liwe safi na muonekano wa kuvutia,ni haya
yafuatayo:
Madoa doa,hayasuguliwi
Pangusa madoa na kitambaa kisafi,paper towels,au sponji.Povu
huondoa madoa kwa kuyafyonza.Kusugua husababisha chembe chembe za uchafu zikae
chini ya carpet fiber,na hii husababisha
uharibifu wa carpet kidogo kidogo.Pendelea kupangusa kuanzia nje ya uchafu
kuelekea ndani ya hilo doa,ukisugua kwa ndani madoa husambaa.
Club Soda
Unaweza kuwa umesikia club soda ina ufanisi dhidi ya madoa
ya kilevi na wine.Ni kweli kama
utaitumia ipasavyo.
Pangusa penye madoa na soda tumia kitambaa.Na kama
haikufanya kazi,changanya 1 kikombe cha white vinegar na 1 kikombe cha maji
weka kwenye chupa ya kupulizia.Pulizia mchanganyiko huo kwenye madoa acha kwa
10-15 dakika yalowane.Chukua kitambaa kifyonze maji na madoa.Rudia mpaka uchafu
uishe.
Pindi uchafu
ukiondoka ,suuza alama za madoa kwa maji ya uvuguvugu.Tumia mkono kubrush kwa
upande wake wa asili.Mwishowe,tandika karatasi(white paper towel) nyeupe safi
kwenye hiyo sehemu wekea kitu kizito juu inaweza ikawa kitabu .Itafyonza uchafu
wote tokea kwa carpet.Iache mpaka carpet likauke,huenda ikawa ni siku nzima. Jaribu Shaving Cream
Shaving cream ya kawaida huondoa aina yoyote ya madoa kwenye
carpet.Weka shaving cream kwenye madoa na iache kwa 30 dakika,pangusa na
kitambaa cheupe kikavu.Malizia kwa kufutia na mchanganyiko wa maji na vinegar
na ufute na kitambaa kisafi.
Kuondoa gum iliyoganda
Umekanyaga gum mtaani hukujua au mtoto kabandika kwa
mazingira yoyote yale,umestukia imeshakua uchafu ulong’ang’ania kwenye
carpet.Fungua freezer lako na chukua vipande vya barafu .Yeyusha gum kwa
sekunde 30.Gum itakua ngumu chukua kijiko kuibandua na itoe kwenye manyoya au
kamba za carpet kama inawezekana,na ulikate kidogo carpet kwa mbali sana na
kama madoa yatatoka hapataonekana.
Sabuni za kuoshea vyombo au za kuondoa grease
Njia nzuri dhidi ya grease na madoa sugu ni matone mawili ya
sabuni za grease au za kuoshea vyombo kwenye kikombe cha maji.Itaondoa mafuta
kama inavyosafisha vyombo.Tia mchanganyiko huo kwa chupa ya kupulizia,
nyunyizia kwenye madoa ya grease kwa carpet,halafu pangusa tena na tena mpaka
madoa yaishe pawe safi.
Nta(Heat Wax)
Mishumaa nyumbani huweza kuangusha nta yake kwenye carpet
,haraka huganda na kung’ang’ania.Hakuna jinsi ni kusafisha tu.Weka pasi kwenye
kitambaa cheupe kwenye madoa aina hiyo,itayeyusha ,tumia kisu cha siagi kuondoa madoa hayo.
Unavyofanya hivyo,weka pasi juu ya paper towel kwenye madoa,nta huyeyuka na
hung’ang’nia kwenye karatasi rudia mpaka nta iishe pawe safi.
La muhimu: Usitumie pasi zaidi ya sekunde 30 hatari kuunguza
carpet.Hakikisha unatumia kitambaa cheupe na white towels,vitambaa vya rangi
vinaweza kuingiliana rangi na carpet wakati wa joto,na zaidi kama una carpet
lenye rangi mpauko,light colors kwa kizungu.
Hydrogen Peroxide
Carpet chache madoa yake ni mfano wa damu na hata damu
yenyewe.Hayaonekani kirahisi
"Hydrogen peroxide itaondoa madoa aina ya damu.Cha
kwanza,utalainisha madoa hayo kwa mchnganyiko wa maji na sabuni kali.Halafu
futa damu hiyo kwa carpet uwezavyo.Ili pawe safi ,tia hydrogen peroxide moja
kwa moja kwenye madoa.Itatoa povu itakapokutana na damu,usishangae.Hapo
utapangusa carpet kwa kitambaa liache likauke.
pipi
Kama una watoto nyumbani,ni muda kabla pipi haijaishia
kwenye carpet.Jaribu kufuta kwa brush au kisu cha siagi,tumia sponji,kwa maji
na sabuni kali.Ni vizuri kuondoa sukari zote kwenye carpet.Kutofanya hivyo
hupelekea hiyo sehemu kuvutia uchafu na wadudu pia.Pindi ukiondoa pipi,kausha
hiyo sehemu na kitambaa safi.
usafi wa kina mara kwa mara(Deep clean)
Kusafisha carpet ni muhimu kwa muonekano mzuri na
mpya.Kusafisha kwa mvuke inajumuisha kutumia dawa za usafi na kuingia ndani ya
carpet kwa kutumia vifaa maalum.Mashine hufyonza uchafu wote kwa njia ya
dawa.Maji yanapenya ndani kabisa ya fiber hadi kwenye floor yani sakafu,huondoa
uchafu mkali na grease zote,na kuliacha carpet lako safi na mshangao wa upya
machoni.
Inashauriwa usafi wa
kina(deep clean) kwa carpet kila baada ya miezi sita kwa familia ya watu wanne.
0 comments:
Post a Comment