Sakamia cleaners imepanga nyumba kadhaa nguo pamoja na
mashuka.Tukagundua njia rahisi ya kupanga kuleta mvuto na muonekano mzuri.Tips
hizi zimesaidia zaidi kwa nguo za linen na nyinginezo. Na imezaa matunda
makubwa mazuri ya kubadili muonekano wa kabati na mvuto pia.Na zaidi haswa
kwenye mashuka
Panga mashuka kwa size
Nyumba nyingi zina aina tatu(3) au mbili za size ya vitanda
na mashuka.Uliwahi kufikiria unaweza kuyasimamisha vizuri kwa bila mategemeo,
ni ngumu kama utavyojaribu.Napendelea rangi nyeupe na cream na kuzipanga kwa
size zake.Zipange sehemu ya wazi au kona kwa size na shepu yake kwa jinsi
ulivyozikunja kuendeana na rangi zake,ni rahisi unapohitaji kutumia na kujua
mpangilio wa mashuka hayo,na husave muda wa kutafuta na kuepusha kupangua.
Weka seti ya shuka ndani ya foronya
Inakurahisishia kuweka seti ya shuka na foronya zake zote
ndani ya foronya moja.Zikunje kwa pamoja kwa mkunjo mzuri zikiwa safi hifadhi
ndani ya foronya.Mazaga zaga yote ya seti ya shuka yatakua pamoja na safi .
Panga mashuka wima(vertically)
Tumezoea kuweka mashuka juu ya lingine.Ni njia nzuri lakini
inasumbua wakati wa kutoa husababisha kuanguka na kuvurugika, haijalishi
umeyapanga vizuri kiasi gani.Ni rahisi lakini inatumia muda mwingi mara kwa
mara utawajibika kupanga.kwa kuyapanga wima huokoa muda na hayapanguki na
rahisi kutoa unapohitaji kutumia.
Tenganisha kwa size na sehemu tofauti
Kujua size ya shuka na size za seti za shuka,panga kila size
upande wake au shelf tofauti.Ni rahisi hata kwa familia kujua shuka ya size
gani ipo sehemu gani bila ya kuvuruga.
Tunathubutu kukuambia kwa mpangilio wa tips hizi za mashuka
umeletaa mvuto wa upangaji na usafi wa hali ya juu.Umesaidia kwa familia
kujitegemea kwa kuchukua shuka bila kupangua na kuhakikisha ni safi pindi
warudishapo.
Tuambie ni njia
gani unatumia kupanga mashuka yako yakaleta mvuto wa usafi?
0 comments:
Post a Comment