Manukato mazuri nyumbani
Kama unaishi na pets au watoto wa kike na wa kiume au hali
ya hewa inakulazimu kufunga
madirisha wakati wote,hapo sasa unatakiwa uifanye
nyumba inukie vizuri muda wote.
Mishumaa ya kunukia,udi,na manukato ya kutengeneza
nyumbaniManukato ya kupulizia,yanaweza kufaa kwa hili.Huondoa harufu ya kila
kitu,na manukato yakiisha ile harufu hurudi tena.Na manukato mengine huweza
sababisha allergies.
Habari nzuri ni kwamba,kwa vitu vidogo unaweza kuifanya nyumba
yako kunukia vizuri.
Wengi wetu hua pua zetu hazinusi vizuri kwa harufi za
nyumbani kwetu,Kama utafanikiwa kujua chanzo cha harufu basi umefanikisha
game.Kwa ujumla tunatakiwa kufuatilia haya maeneo majumbani,eneo moja badala ya
jingine na kusafisha kila mara .
Jikoni:
Hakikisha la
kutunzia uchafu safi.Kuwa na tabia ya kusuuza mfuko au kifungashio cha nyama
kabla ya kutupa,na vitu vyenye harufu kali vyote.
Safisha la kutunzia taka kila wiki na ikiwezekana kila
uoshapo vyombo.
Hamna la kuhifadhia taka?mabomba ya maji taka ya jikoni
husababisha harufu pia.
Hata kwa matumizi ya kila mara,uoshaji wa vyombo huleta uozo
na mabaki ya vyakula yananasa kwenye bomba husababisha kunuka.Safisha
dishwasher angalau kwa mwezi mara moja. Hakikisha harufu mbaya haitokei kwenye hifadi au dishi la
vyombo.
Chumba cha kulala:
Hivyo viatu vya
tennis au malapa unayotumia unavua kabla ya kulala huenda navyo vinatoa harufu
nyumbani au chumbani.Safisha viatu vinavyonuka,kama ikiwezekana,au jaribu njia za kutoa harufu na uchafu wa viatu.
Kuna kikubwa chumbani
kwako ndo sababu kuu ya kunuka.Safisha godoro ili kuondoa harufu ya
majasho,ukungu,uvundo,n.k
Sehemu ya kufulia
Sabuni ya kufulia
na mafuta ya mwilini hujenga uchafu kwa mashine ya kufulia hata mabeseni
pia,huleta harufu mbaya.Hata kama unatumia karo bado nalo hutoa harufu
mbaya.
Uvundo na mchanganyiko wa masabuni husababisha harufu mbaya
nayo yahitaji kusafishwa.Isiposafishwa kwa muda mrefu husababisha hata nguo
kunuka.
Sebuleni au makazi ya family
Pets huwa wanaruka kwenye furniture;wanaacha uchafu na
kiarufu flani hivi.Usiache kusafisha uchafu kuzifanya furniture kuwa safi
wakati wote.
Vitu vingi vinavyoleta madoa kwa carpet
husababisha harufu pia.Safisha madoa kwenye carpet ikiwezekana tuite Sakamia ni
wataalamu wa fani hizo.
Hata kama carpet lako halina madoa bado linabeba harufu na uchafu wa kukanyagwa na miguu.Kusafisha ni
muhimu.
Chooni/bafuni
Kitu kimoja kikuu kinachosababisha harufu sio watu: ni
uchafu ndo sababu kuu.Safisha showers na tub kwa harufu nzuri.Patunze
kusichafuke tena.
Kama sehemu za juu ya meza ndani ya vyumba vya
kupumzikia,rugs za bafuni,nazo huchafuka sana.Sababu zina kuwa na unyevunyevu
mara kwa mara,ni rahisi kutengeneza ukungu na huleta harufu mbaya,pia.Safisha
rugs za chooni kila wiki.
Of course, choo
kichafu na utelezi au uchafu wa bafuni lazima huleta harufu.Tumia sabuni za
kuua vijidudu za asili kuondoa harufu kila wiki,usafi wa kufuta na kupaacha
pakavu kila mara,kuliacha bafu au choo kikiwa safi na harufu nzuri.
Chunguza ukuta wako usiwe na ukungu,pia,kama hauna feni
chooni kwako,hii najua kwa mazingira yetu vyoo vingi havina feni ,kwahiyo ni
kukomaa na usafi wa hayo maeneo.
Kumbuka,kusafisha mara kwa mara itasaidia kuondoa harufu
kuliko hiyo mishumaa ya harufu au manukato yoyote kwa kunukia vizuri.
Jipangilie vizuri na muda wako kupata nafasi ya kusafisha nyumbani kwako.
Jipangilie vizuri na muda wako kupata nafasi ya kusafisha nyumbani kwako.
Be Hygienic and Smart!
0 comments:
Post a Comment