• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, August 24, 2021

MAMBO 11 YASHANGAZAYO

12:51 AM // by Kalma // No comments

 MAMBO 11 YASHANGAZAYOVitu vya nyumbani vinavyotumiwa kama bidhaa za kusafisha

Unaweza kukata tamaa kugundua ya kwamba au umesahau ukajikuta huna dawa za kusafishia wakati una mzuka pindi umeutamani mng’ao nyumbani kwako. Usifadhaike! Wafanyabiashara hawa wa kushangaza wa nyumbani kwako watakuokoa na kukufurahisha. Na (ziada!) Wao ni bora zaidi kwenye mazingira, na nyumba yako kuliko kemikali kali zinazopatikana katika maeneo ya manunuzi.D

awa ya meno(Toothpaste)Dawa ya meno inayotumika kwa usafi.Kutoka pumzi ya harufu 

ya minty kung’arisha mapambo ya silver na dhahabu,na kuweka maeneo ya kuzunguka nyumba yako na kuyaacha kwa mng’ao:

Mabomba na vifaa vya stainless steel bafuni.

Huondoa mgando wa sabuni milango ya chooni au bafuni

Huzuia vioo kuweka ukungu.

Husafisha kifaa cha kunyoosha nywele.

Hung’arisha funguo za piano.

Husaidia kufifisha mikwaruzo ya screen ya simu ya mkononi.

Juisi ya Ndimu

Nje ya jikoni  achilia mbali kiungo pendwa, maji ya limao huondoa  madoa ya asili, hung’arisha fanicha, na kusafisha glasi

Hung’arisha aluminium, chrome, stainless steel, na shaba.

Huondoa madoa kwenye counter tops za aina ya tiles.

Husafisha coffee maker na mabuli (kettle) ya maji au chai.

Huondoa madoa ya chakula kwenye vyombo vya plastiki na sahani.

Huua bakteria na harufu kwenye ubao wa kukatia wa aina za mbao.

Huondoa madoa ya njano, kutu na ukungu kwenye nguo.

Changanya na mafuta ili kuleta mng’ao kwa fanicha.

Hung’arisha vases za glasi, madirisha ya vioo. 

Mafuta ya Nazi

kijiko cha mafuta ya nazi

Tumesikia juu ya maajabu ya mafuta ya nazi yasiyo na mwisho utasema uchawi. Angalia mwenyewe jinsi mafuta yenye miujiza ya kweli!

Husaidia kutunza bawaba ya mlango.

Hutumika kuondoa lebo kwenye jagi aina ya glasi.

Hung’arisha fanicha ya mbao.

Ina fifisha michirizi kwa mikoba na viatu vya ngozi.

Huondoa michirizi kwenye vifaa vya chuma cha pua.

Husaidia na kulainisha wakati wa kukwangua utomvu wa miti, kinyesi cha ndege, na mende waliokufa bila kuharibu rangi kwenye gari lako.

Changanya na baking soda ili kusugua mabaki ya sabuni kwenye milango ya bafuni.

Ketchup

Kijiko cha ketchup

Ipende au ichukie, ketchup ni nzuri kwa zaidi ya kwenye chips au hot dog.

Hung’arisha silver,sufuria za shaba na dhahabu pia.

Baada ya kuosha gari lako, ipe mng’ao wa haraka na ketchup.

 coffee ground

Njia yetu tunayopenda kutumia coffee ground ni kwenye bustani. Jifunze juu ya faida zote za coffee ground kwani ni yenye mazingira rafiki na hupendezesha eneo!

Nyunyiza ndani na nje kuzuia wadudu wasiohitajika.

Hunukiza eneo la takataka kwa  kijiko kikubwa kimoja  cha coffee ground.

Kuongeza ukuaji wa mimea inayopenda asidi kama azaleas, blueberries, na waridi.

Huondoa harufu ya vitunguu mikononi na cutting board.

Tea Bags

Unapendelea chai kuliko kahawa? Fuatilia hapa:

Huleta mng’ao  kwa sakafu ngumu kwa kutumia chai.

Huondoa harufu ya mabaki ya vyakula ndani ya friji au friza.

Hupaacha safi  ndani ya microwave kwa kutumia tea bag ilyolowa au hata kavu.

Huondoa madoa kwenye toilet bowl

Tumia tea bags  ya chai iliyotengenezwa au isiyotengenezwa kwa kung’arisha vioo vya madirisha.

Tumia tea bags kavu kwa kufyonza harufu katika viatu vinavyonuka.

Hydrogen Peroxide

Ikiwa huna chupa ya hydrogen peroxide kwenye hazina zako za dawa za usafi, sasa ni wakati wa kuwa nayo na kuhifadhi!

Hung’arisha nguo nyeupe kama m-badala wa ukali wa bleach.

Huondoa madoa ya damu,rangi ,berry,na hata madoa ya ukungu kwenye nguo.

Disinfect mashine ya kufulia nguo kwa kuongeza kikombe kimoja ndani ya mashine ikiwa haina nguo, iache izunguke na maji moto.

Cornstarch

Bakuli la unga wa cornstarch

Je! Unapenda kuvaa gloves za mpira?wakati wa pirika na ubusy?Pakaa cornstarch na utushukuru baadae wakati wa yafuatayo:

Huondoa  madoa ya grisi kwenye nguo, zulia, na upholstery.

Mchanganyiko wa maji na cornstarch hung’arisha silver.

Huondoa madoa na kumtakatisha hata wanyama pia.

Huzifanya gloves za mpira kuwa nyepesi na huondoa harufu na kujisikia vizuri utumiapo.

Huondoa madoa ya mafuta kwa sakafu.

Mchanganyiko wa kipimo kimoja cha maji na viwili vya cornstarch husafisha vizuri tops za vioo kwenye jiko.

Husafisha na kuyaacha na harufu nzuri magodoro na mito

Olive Oil

chupa ya olive oil

Kama wapishi wote wa nyumbani tayari wanajua, mafuta kidogo ya olive oil hufanya mengi.

Kusugua vifaa vya kupikia vya chuma (frying pans) kwa kuweka mafuta na chumvi. Suuza tumia maji ya moto na kausha vizuri.

Huondoa rangi  mikononi na ya dirisha za glasi kwa mafuta kidogo, ikifuatiwa na sabuni au kusafisha madirisha.

Punguza mikwaruzo kwenye fanicha aina ya  ngozi kwa tone la mafuta kwenye pamba ng’arisha na kitambaa laini.

Hung’arisha vifaa vya chuma kwa mafuta kidogo, tumia kitambaa laini.

Andaa  polish kwa ajili ya fanicha kwa vipimo viwili vya olive oil na kipimo kimoja cha maji ya limao

Fanya viatu vya ngozi vya patent kung'aa na tone la mafuta na ung’arishie nguo kwa haraka.

Tone moja kwenye cotton buds pakaa kwenye meno ya zipu,italainisha na kufunguka kwa urahisi.

Baking Soda

Baking soda kwa usafi wa majumbani!

Watu wengine huapa kwa baking soda kama bidhaa ya kusafisha uchafu kama wote. Ukishaijaribu,huwezi kuacha kutumia .

Husafisha ukungu wa sabuni kwenye bath tub,milango ya vioo bafuni ambavyo vinaweza kuchubuka iwapo itatumika dawa kali za kusafishia.

Huondoa harufu kali ya jasho, ukungu, na manukato ikitumika kufulia.

Huleta harufu nzuri kwa gari lako.

Husaidia kwa kuondoa mabaki ya mchanga na sabuni kwenye vitambaa kwa kuongeza kikombe kimoja cha baking soda wakati wa kusuuza.

Utapenda muonekano wake mfano wa kuchemka ! Changanya sawa kwa sawa kipimo cha baking soda na white vinegar kwa kusafisha vya kuhifadhia taka.

white vinegar

White vinegar kwa sehemu au chumba cha kufulia ni kama siagi ya karanga kwenye mkate au mboga. Zifuatazo njia ambazo unaweza kusafisha na white vinegar:

Ng’arisha nguo nyeupe na ukate harufu kali kwa kuongeza kikombe cha white vinegar kwenye maji wakati wa kusuuza.

Hulainisha au kufuta mistari ya pindo kwa kutumia kitambaa kilolowekwa na white vinegar weka juu ya nguo kwenye pindo wakati wa kupiga pasi.

Huondoa au kukata mafuta kwa dishwasher kwa kuongeza kikombe kimoja cha white vinegar yenye vyombo au isiyokuwa na vyombo wakati wa mzunguko, vifuniko vya kupika, na vifaa vidogo vingine.

Huondoa magugu kwa kupulizia juu ya magugu hayo kwa bustani.

Huondoa stika kwa usalama kwa kuinyunyiza white vinegar kwa vifaa mbalimbali.

Huondoa harufu hata moshi wa rangi kwa kuweka bakuli lenye white vinegar kwenye chumba baada ya kupaka rangi.


Share! Like ! Comment !

Be Hygienic ! Be Smart !
 


0 comments:

Post a Comment