• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, October 6, 2013

USAFI WA KUCHA

1:21 AM // by Kalma // No comments

USAFI WA KUCHA

Kucha za vidole zina mvuto sana. Zinaoneonekana unapotoa Hello, unaposhikana mikono,kwenye interview,kazini,na kumuonyeshea mtu kitu.

 Unafikiri kucha zako zinakuambia nini?
Kama ni chafu hazitunzwi zinatuma alama duniani kote kwamba; Hauna muonekano mzuri!.
Ziweke kucha zako safi mara zote.
Ijumaa(Friday) ni sikukuu,vizuri upendeze kwa muonekano wa kucha safi na nzuri .
   Mimi na familia yangu siku hii ndo tunakata kucha na kuziacha zikiwa safi na zenye afya.

                      JINSI YA KUSAFISHA KUCHA.
 Wekeza vifaa vizuri vya kisasa vya kutunzia kucha.
Tumia brush ya kucha kwa kusugua chini ya kucha na kuutoa uchafu na kufikia sehemu ngumu ambapo uchafu unajilundika. Unaweza tumia mswaki ukiwa huna vifaa vya kisasa.
      Tumia maji moto na sabuni ya kunawia mikono.Anza kwa kusugua chini kabisa kwa kushikilia brush chini na sugua kuanzia nyuma kuja mbele pole pole, kisha juu ya kucha fanya hivyo kwa kuzunguka.

      Toa rangi kwa kuloweka pamba kwenye polish remover na usugue.kwa vidole vyenye hinna huna haja ya kuitoa. kwa vidole vya afya na nguvu vipumzishe kwa kutumia polish kila baada ya wiki kadhaa.
       
         Loweka kucha na maji kwenye bakuli,au sinki,au kifaa cha uwezo wako hata dishi poa,kwa maji ya moto ya uvuguvugu na pitisha sabuni ya kunawia mikono.Na ni kucha tu usiloweke mkono mzima,kwa dakika tatu,sabuni kwenye maji hufanya mikono kuwa mikavu .
  Uwe ndo muda wako wa kupumzika ongea na watu,angalia tv,cheza na baby afterall akiwa mtoto mtundu atashika hichi,avuruge hapa, atie mkono kwenye maji, na huwezi kumnyang'anya basi ndo rahaa zenyewe hizoo.
          
            Suuza kwa maji ya bomba ya uvuguvugu,au yalokua kwenye chombo yaani jimwagie,kisha zifute na taulo laini.

       Kisha tumia kikatio kucha kukata maana zitakua laini,au kifaa cha kuzipunguza kuweka sawa kama hauzikati.
      Unaweza kuzitunza kucha zako zaidi kwa kutumia"Sally Hansen Hard" kwa usafi,kutunza,na zenye nguvu. Hii ni kama tiba ya kucha "Nail clear tretment"!.
 
Inashauriwa baada ya kukata kucha chimba shimo dogo tu uzifukie, sio desturi nzuri kutupa tupa kucha hovyo.Jua kucha ni uchafu pia.





0 comments:

Post a Comment