• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Sunday, October 20, 2013

WAXING

5:58 AM // by Kalma // No comments

Mng'aro au waxing ni mchakato,mfumo wa kutoa nywele unaotolewa kwa kutokea mzizi wa nywele. Nywele mpya huchelewa kuota kwa wiki mbili hadi nane,japo wengine huweza kuwahi kuota hata wiki moja.Waxing huweza fanyika sehemu au kiungo chochote cha mwilini,ikiwemo nyusi,uso,kwapani,miguuni,mikononi,mgongoni,kifuani, n.k.

  Ziko aina nyingi za waxing; 

Strip waxing

Hii ni ile hupakazwa au kupuliziwa eneo la ngozi,huwekwa nguo au karatasi na kutolewa kwa kinyume.Hii hufuata njia za nywele. Kuepusha "trauma" ya ngozi.

 Hii unaweza tumia maji ya ndimu,asali na sukari.

 Strip-less wax

Hii ngumu hutolewa bila nguo,huwekwa ikiwa imepoa,hutumika zaidi kwa wale sensitive skin.Inashauriwa waxing ya sehemu sensitive kutumia zaidi wataalam wa shughuli hizo Cosmetologist or asthetician. Sehemu zote za mwili huweza fanyia waxing,ikiwemo pua na masikio.

Eyelashes na eyelid hizi ni hatari kuzifanyia waxing.Waxing huweza fanya kwa matayarisho ya kupakaa hinna kwa mikono na miguu.

Halawa ni neno la kiarabu linomaanisha waxing.

Kawaida jambo huwa lina faida na hasara. Waxing pia ina faida na hasara.

     Faida;Hutoa nywele nyingi kwa muda mfupi.Hukuacha soft na mng'ao mzuri.Nywele hazioti haraka makadirio wiki nane .Dipilatory cream huondoa nywele za juu juu haitoi mizizi .Husababisha nywele kuota haraka na hovyo hovyo.Haitengenezi weusi wa njia za kiwembe haswaa kwapani.

Hasara;

Waxing ina maumivu ya ngozi.Huweza leta madhara ya ngozi pia.Ni ghali na gharama.Ngumu kujifanyia mwenyewe sehemu nyingine za mwili kama mgongoni.Wenye asili ya kutokuwa na nywele waxing husababisha kutoota kabisa .

TIPS.Hakikisha urefu wa nywele ni 1/4 inch hadi 8 inch.Iwe umekaa wiki nne baada ya waxing. Hautumii dawa ya ngozi au yenye madhara na ngozi.Haukuwa na mazoezi magumu ndani ya saa 24 kama kuogelea.Weka mahala pa kufanyia waxing safi na kavu.Oga maji moto.Usipakae cream,gel,hata mafuta husababisha nywele zisitoke.Usinywe pombe.Unaweza kunywa dawa za kutuliza maumivu kabla kwa dk 30-45 kama Ibuprofen.

           JINSI YA KUTENGENEZA/HALAWA.

Sukari robo kilo.Maji ya limao au ndimu.Kitambaa cotton au waxing paper. Koroga sukari kwenye maji ya ndimu ikikorogeka vizuri ichemshe mfano wa shira isiwe nyepesi wala nzito sana .Iache ipoe isiwe ya moto, pakaa kitambaa weka sehemu husika na iache kwa dakika chache bandua .Weka viganja vya mikono kama unapooza maumivu halafu pakaa powder.Unaweza mfanyiabi harusi na hata wewe mwenyewe. Huweza kutumika saluni ukiwa na kile chombo cha kuchemshia.

ILANI.
   Pata ushauri wa daktari kwa matumizi ya dawa aina yoyote.

 ENJOY !











0 comments:

Post a Comment