• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, October 2, 2013

KUKU

2:11 AM // by Kalma // No comments

KUKU

Kuku ni ndege, Poultry kwa dunia nzima.

Kuku anaandaliwa kama chakula kwa upana tofauti, kutofautiana na mikoa,miji, na utamaduni pia.Nakumbuka zamani imani ya wengi ilikua kipaja,zile firigisi anakula baba tu nyie wengine mnakomaa na vipapatio, shingo, afadhali siku hizi mila hIyo naona imekoma. Hahaha.... unaikumbuka hiyo?  Nyama ya kuku ina mafuta,vitamini tele za kutosha,afya ndo mwake.Kuku unamswanifu unavotaka ana mapishi tofauti lukuki, supu,wa kukaanga,kuokwa, boneless, hutiwa rangi uipendayo akaitwa : kwa kijiwe vya chipsi kuku wekundu, tanduri, ilimradi ndege huyu anapendwa na kusifika kwa  majina yake tofauti.

Nakwambia na ladha yake haswaa tamu .Nyama yake ni nyeupe.  Wako kuku wa kienyeji, wa kizungu, chotara,kuchi n.k.

  Supu ya kuku nzuri kwa mama aliejifungua asubuhi mapemaa ikiwa ya moto inatia mwili joto na kutengeneza maziwa ya afya kwa mtoto.


 Achana na hilo mimi binafsi napenda kuwaandalia familia yangu kuku aina hii; 
Nikishamkata kata kuku,naandaa viungo yaani tangawizi,thoum navitwanga pamoja, kitunguu maji nakata pembeni, Pilipili hoho, karoti, pilipili mbuzi kidogo, ndimu na chumvi kiasi.
Natia kuku kwenye sufuria naweka hivyo viungo vyote kasoro karoti na hoho.  Ukiweka mapema vinalainika haraka.

Vikiwa vizima vitamu zaidi.Kisha nakaanga kuku yenyewe inajichuja maji nakoroga na mwiko,maji yakikaukia natia nusu kikombe cha maji,kwa dakika kadhaa,ikianza kukaukia inajichuja mafuta.

Nakaanga kwa hayo hayo mafuta natia hoho na karoti ikikaangika na inakua na harufu nzurii .Hiyo kwa mkate wa manal ,pembeni chai yako ya viungo, tango umelikata umetia chumvi kwa mbali wee tamuuu. Au kwa tambi za sukari.

Familia yangu hufurahia mlo huo wanajisikia haswa mtoto Ayyani anaenjoy sana hiyo, mr. pia hufurahia. Jaribu hivo leo utaniambia. Halafu huchoki sababu hukai jikoni sana .

Hata kwa wageni huwa ni kitamu.

Hivi kweli  wanawake wanapenda zaidi kuku kuliko wanaume?
    Hahaha....nimesikia kucheka mimi napenda sana kuku, mama yangu,mama mkwe wangu,dada zangu, wanangu,na rafiki zangu .....itakua kweli eeehhh....!!!


















0 comments:

Post a Comment