• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Thursday, October 10, 2013

MAHARAGE (BEANS)

1:24 AM // by Kalma // No comments

MAHARAGE (BEANS)

Maharage ni mbegu inayopandwa. Chakula kwa binadaamu hata wanyama.

Kwa familia zote pia.

Maharage ni mboga ya vitunda au vimbegu, yote ni sawa tu.Ni zao la biashara sana.Sokoni kokote huwezi kosa maharage duniani .

Mimi nayapenda sana maharage ya Mbeya nahisi ndo mazuri matamu na  yanakolea nazi. 

Ni kisababishi kikubwa cha Protein tokea enzi mpaka leo tena duniani kote. Duniani kabila nyingi na vitongoji vingi mbalimbai, hupanda maharage na mahindi nyumbani, ni yanavutia sana kwa sababu hii:

 Maharage yana "Heliotropic"majani yake yanachanua mchana kushabihiana na jua lakini usiku nayo yanalala!  Soo interesting!.

Aina za maharge ziko 40,000 elfu arobaini duniani kote.

 Toxin(sumu)inayopatikana kwenye maharage mekundu na kidney beans unaweza ukaita "maharage ya figo" yana madhara huondolewa kwa kuchemsha .Inashauriwa kuyachemsha kwa dakika kumi(10).

Ukitumia slow cooker sababu ya temperature kidogo,sumu haitatoka vizuri na hata maharage yenyewe hayatakua mabaya wala hayatakua na harufu, pia sio tatizo ila sumu hiyo itakuwako kidogo.

Cha kufanya ni kuchemsha kwa moto mkali wenye temperature kubwa kwa muda wa dakika kumi yawe yameiva.

        Fermantation inatumika sana sehemu ya baadhi ya Afrika kwa kuongezea afya nzuri ya maharage na kwa kuondoa sumu pia.
     Kenya,Malawi,Tanzania,Uganda ,na  Zambia maharage ni sababu kubwa ya mlo bora kwa protein.
Ina nyuzi "fiber" ya kutosha ambayo kikombe kimoja cha maharage inapatikana kiasi cha gm 9-13 za fiber.

Soluble fibre inasaidia kushusha blood presha,na cholesterol.

Maharage yana protein,wanga,folate,na madini ya chuma kwa sana tuuu.
Soya beans ni maharage yalopewa sifa kuongoza kwa virutubisho zaidi.Japo yote ni mazuri na yana virutubisho ila SOYA BEANS yanashika namba.


 Mkakati wa maharage fanya hivi; Loweka kwenye Baking Soda na hata kuoshea hii baking soda.

Muda mwingine tumia Vinegar baada ya kumaliza kuyapika kwa kunyunyizia juu, huyafanya maharage kuwa laini zaidi.

Tangawizi ukichemshia au ukiungia wakati wa kupika maharage hupunguza kasi ya gesi na sumu pia.

Na ile sijui siku hizi ipo Magadi ukichemshia nayo yanakata makali ya sumu.

Maharage yana gesi kama hayatalowekwa na kuchemshwa vizuri. Ndo hapa kwa wenye vidonda vya tumbo wanaambiwa wasile,ila ukifanya hivo kwa vizuri sio mbaya na hayataleta madhara sababu gesi utakua umeiondoa.


   India wanaongoza kulima maharage, wakifuatiwa na Brazil, na Myanmar.
     Afrika anaongoza Tanzania kwa kilimo cha maharage na nafasi ya saba duniani.
   Kiukweli ni chakula cha rahisi kila mwenye nafasi huweza kukimili chakula hiki.

  Mimi binafsi napenda maharage ya nazi kwa ubwabwa,na juisi flani hivi na ndizi mbivu. Duuh!.....



0 comments:

Post a Comment