• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Monday, October 14, 2013

KUOSHA USO KWA ASALI

12:34 AM // by Kalma // No comments

ASALI USONI

Asali ni asili yenye vitu vingi kwa ajili ya ngozi yako .sio kama cleanser za kibiashara zenye wingi wa sumu za dawa,ambayo hutopenda mwili wako utumie.

Asali yenyewe halisi ile safi hulinda na vijidudu na hufanya kazi ya ukwee kusafisha ngozi yako, na kukuacha bila mikwaruzo.Jinsi ya kuosha uso;

Nawa mikono yako vizuri. Chovya mikono yako kwenye asali kisha pakaa usoni.unaweza ukaipasha kidogo kama ni kavu sana juu ya maji ya uvuguvugu kwa mbali na isiwe ya moto,yaani kama kuilainisha. Waweza kupakaa uso ukiwa mkavu au ukapakaa maji usoni kisha ukapakaa asali, ila hii ya kulowesha uso nzuri zaidi.weka kwa dakika tano(5)hadi kumi (10),hii haina haswaa dakika kamili za kuweka hutegemeana na nafasi ya muda wako.

Kama una nafasi haina mbaya,kama ile ya asubuhi ya kuendea kazini nayo utajipima na nafasi yako.Ni vizuri kupakaa asali kabla hujapiga mswaki.Suuza uso na toning unayotumia.Pia kuosha bila cleanser ni nzuri zaidi.

Inashauriwa kutumia maji baridi sababu asali ina leta joto ambalo linafungua vinywelea, na ili vinywelea vijifunge maji baridi ndo mazuri kufungua vinywelea. Futa na taulo laini la uso.

Asali ina tengeneza uso kuwa;Laini na nyororo.Haikaushi uso kuwa mkavu. Ina ua vijidudu kutokea kwenye vinywelea(pores).Asali haiathiriwi na joto.Ni rahisi na hutumia muda mfupi.Hukausha pimples na vipelepele. Inapoteza mabaka na makovu. 

Ni nzuri kwa ngozi aina zote,zenye mafuta ,kavu,n.k.

   FACIAL YA ASALI NA MANJANO 

Powder ya 4*4 Kijiko cha chakula kimoja cha manjano,kijiko cha chakula kimoja na nusu cha asali,kijiko cha chai kimoja cha powder,nusu kijiko cha chai cha maji ya ndimu. Changanya kwa pamoja,vichanganyike vizuri pakaa usoni.Muda dakika kumi(10) na kuendelea,hutegemea nafasi yako.

Ndimu hufunga vitundu vilo wazi usinyemelewe na vijidudu na hulinda na upele.Hii ni sawa na mask,cream,kama lotion pia .

Hupendelea kutumia hii facial nikiwa na mtoko wa ukwee,uso hependeza ukipakaa make-up.Ni nzuri kumuandalia bi harusi  kwa muonekano mzuri apakaapo make-up.

Manjano hii hutumika kuleta rangi nzuri ya uso, ni bleach ya asili.
    Imezoeleka ukitaka pakaa bleach usoni ili iwe nzuri unatoa vinyweleo ambayo sio nzuri kiafya .
Manjano, huitaji kutoa vinyweleo na hukuacha uso uking'aa. Ni nzuri kufanya kwa wiki mara moja.

Hii pia huweza kupakaa mwili mzima kujisugulia(singo).Hutoa uchafu na hulainisha ngozi.






0 comments:

Post a Comment