• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Tuesday, October 22, 2013

FACIAL YA NDIZI

8:06 AM // by Kalma // No comments

FACIAL YA NDIZI

Ndizi ni exceptional kwa vyakula vya afya.Na iko vizuri kwa urembo wa uso.
     Ndizi ina numerous za kutosha,ni tunda lenye Vitamin A,B,C na E na madini kama Chuma,Manganese,Zinc,Potassium.Kula ndizi kuna manufaa mengi sana mwilini hutengeneza shape nzuri, unapoila hutengeneza nywele na ngozi huziweka katika hali nzuri.
     
       Ndizi ina Vitamin C na B6 kwa ngozi.Antioxidants na manganese iliokuwepo hulinda ngozi isiharibike  na oxygen kutokana na temperature na kupambana na kuzeeka kwa ngozi,hufanya ngozi kuonekana ya kitoto na nyororo.

      Ndizi ni kilainisho asili(natural moisturizer).
Ndizi hurekebisha wepesi(iloregea) na ukavu wa ngozi.Kwa kusaga na kupakaa usoni.
          Ndizi nusu, changanya na kijiko kimoja cha kula cha maziwa ya mtindi na kijiko cha kula kimoja cha mafuta ya Vitamin E. Pakaa usoni kwa dakika 30 kisha nawa na maji ya uvuguvugu.


    Ndizi kwa mng'ao wa ngozi na mwanga.Kwakuwa ndizi ina Vitamin C husaidia kuiweka ngozi kuonekana yenye mng'ao na mwanga,na kuifanya ngozi kuonekana ya kitoto.
             Nusu ndizi changanya kijiko 1 cha kula cha msandali au sandalwood powder,nusu 1/2 kijiko cha chai cha asali pakaa usoni kwa dakika 20-25 osha na maji vuguvugu .
  Hii ni kwa ngozi yenye mafuta, sandalwood husafisha Sebum na mafuta yalozidi wakati ndizi hulainisha ngozi.
               AU
        Ndizi moja changanya na maji ya ndimu vijiko vya kula 2-3 pakaa usoni kwa dakika 25.Hii huondoa spots na vilema kwa Vitamin C yake iliokuwepo na husaidia kuondoa ngozi ilonyauka.

        Ndizi kwa kusugulia uso (Scrubing).
Ndizi moja,sukari kijiko 1 cha kula,changanya vizuri pakaa usoni na sugua kwa upole,Ndizi hulainisha ngozi kavu na sukari huondoa chembe mfu kwenye ngozi.
         Ndizi moja isage na Oats vijiko vya kula 2-3,na kijiko cha kula 1 cha asali,kijiko kimoja cha kula cha maziwa.Pakaa usoni kwa dakika 15 kisha sugua.Osha na maji baridi kwa ngozi kavu sana,unaweza usitumie maziwa ukatumia fresh cream ya maziwa.
           Ndizi nusu,kijiko 1cha kula cha tui zito,vijiko 2 vya kula vya mchele saga kwenye blender sugua uso na kisha osha na maji uvuguvugu.


            Ndizi 2 na strawberies 4-5 saga kwenye blender,vijiko 3 vya sukari vya chakula, jisugulie mwilini pindi unapotaka kuoga.
    Hii scrubin ni nzuri kwa bi harusi mtarajiwa anapokua ndani kwa maandalizi ya harusi.

        Ndizi kwa ajili ya kupambana na kuzeeka kwa ngozi. Hupambana na makunyazi na kuweka ngozi kama ya mtoto.Mask ya ndizi; changanya Vitamin A na E na Avocado pakaa usoni kwa dakika 25 na osha uso. Hufanya ngozi kuwa laini nyororo na hutibu kuharibika na free radicals.
            1/4 ndizi na kijiko cha chai cha maji ya rose pakaa usoni mpaka shingoni kwa nusu saa,kisha osha .Hulainisha ngozi .

         Ndizi kwa kulainisha miguu,husaidia kuweka nyayo soft na huondoa mipasuko ya miguu(makenya).saga ndizi mbili pakaa kwenye nyayo kwa dakika 10 osha kwa maji moto.husaidia kulainisha nyayo kavu.

            Ndizi kwa Puffy eyes,saga ndizi na pakaa chini ya macho huitwa miwani ni weusi unaotokea chini ya macho, kwa dakika 15-20 na osha kwa maji yalopoa sio moto sio baridi,cool water.


    Husaidia kuondoa mvimbo wa chini ya macho,hii hutokea sana pindi ukichoka sana na usingizi usoisha.Huondoa weusi na kuvimba kwa Potassium ilokuwako kwa ndizi,unaweza tumia maganda ya ndizi pia.

   Jiangalie mwenyewe, Ndizi ina faida nyingi mwilini.  Haswaa kwa Urembo ngozi na mwili kwa pamoja .Ina virutubisho vitakaotengeneza mwili wako uwe wa afya na muonekano mzuri.

    Huna budi kutumia ndizi kwa mlo wako mmoja kwa siku.
Ndizi ni rahisi kupatikana kokote .
Kama unaangalia jinsi ya kusave hela na kuwa mrembo achana na madawa yasiyo muhimu, ndizi ni suluhisho lako wewe, na familia yako.
   Kwa mtoto ni nzuri kwa kumeng'enya chakula haraka na rahisi kuitafuna .
Unangoja nini? Kwa urembo na afya ya mwili ni ndizi tuu.














0 comments:

Post a Comment