• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, October 9, 2013

KUNYONYESHA(breastfeeding).

3:54 AM // by Kalma // No comments

KUNYONYESHA

Utaalam wa kunyonyesha ni special kwa sababu nyingi furaha ya muunganiko kwa mama na mtoto,unapunguza gharama, na faida za kiafya kwa mama na mtoto.


     Umuhimu wa kunyonyesha;


Maziwa ya mwanzo huwa ni ya rangi ya gold.

  Haya yana colostrum ni membamba texture yake yanatengenezwa kipindi cha ujauzito na mara tu baada ya kujifungua,yana virutubisho na kingamwili za kutosha kwa kumlinda mtoto.Japo mtoto anapata kidogo lakini yanamtosha kwa tumbo lake.

 Yanabadilika pindi mtoto anakua
            Colostrum hubadilika vile mtoto anavokua na yanakomaa huitwa "mature" milk, kwa siku tatu(3) hadi tano(5) baada ya kuzaliwa.yana mafuta,sukari,maji na protein kwa wingi husaidia kwa ukuaji wa mtoto.Ni membamba laini kushinda colostrum yana virutibisho vyote na vilinda mwili kwa saana.

   Maziwa ya mama yanabadilika kadri mtoyo anavokua.
             Kwa watoto wengi haswa(njiti) premature, maziwa ya mama ni rahisi kuyeyuka kuliko ya kopo.Protein ilokuwako kwenye maziwa ya kopo haya yanatokana na ng'ombe yanachukua muda mrefu kuyeyuka kuendeana na mfumo wa kuyeyusha chakula kwa mtoto.

  Yanapambana na vijidudu

Celi, homoni,na kingamwili ni kwa maziwa ya mama. Hulinda kwa upekee huwezi fananisha na chochote. Ni kinga ya maradhi kwa mtoto. Maziwa mengi ya kopo yana athari kwa masikio,kuharisha, Necrotizing enterocolitis hivi ni aina ya vijidudu vyenye madhara kwenye njia ya utumbo kwa watoto wachanga.
Yanadhoofisha mfumo wa upumuaji. Huweza sababisha athma(pumu).
Obesity aina ya pili (type 2) ya kisukari.

Wachunguzi wamesema kunyonyesha kuna punguza athari pia ya kisukari,leukemia, ugonjwa wa ngozi kwa watoto,na vifo vya watoto pia.
Usisahau kufa ni siri ya mungu pekee ndo ajuaye.

            FAIDA KWA MAMA ANAENYONYESHA.
Maisha yanakua mepesi na rahisi.Huna haja ya kununua chupa na kuosha pia,kununua maziwa ya kopo,huamki usiku kuandaa,na kuchemsha chupa.
                Inapunguza gharama ya pesa na mtoto kuumwa umwa.
                Hujenga mapenzi na mawasiliano baina ya mama na mtoto,humjengea mtoto joto,ulinzi,kujiamini na kujisikia murua.
                Humlinda mama na cancer ya matiti,cancer ya ovaries, kisukari,na unyogovu baada ya kujifungua.
                kupungua uzito .
               Muda wa kupumzika kutokana na dharura mbalimbali ofisini,mfano kupeleka mtoto clinic n.k.

              FAIDA KWA JAMII.
Taifa linahifadhi hela za budget ya dawa za kutibia watoto kwa asilimia kubwa tu.
Inapunguza vifo vya watoto.
Inaongeza nguvu kazi zaidi,sababu wa mama wengi watazalisha kwa kutokuwa na watoto dhaifu.
Huyalinda mazingira kuwa safi wakati wote kwa kutotupa ,uchafu wa makopo,mifuko,maganda,n.k.

Haisumbui kwa mtoto anaenyonya kupata maambukizi ya magonjwa ya mlipuko,kama yanayosababishwa na maji.

    
       








     

            




0 comments:

Post a Comment