• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Friday, October 4, 2013

VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)

3:25 AM // by Kalma // No comments

VIDONDA VYA TUMBO (ULCERS)

Kuna aina nyingi ya ulcers moja wapo ni vidonda vya tumbo,  ipo ya mdomo, pressure, stress,na ya ngozi .

Ulcers kwa maana ni kukatika kwa mfumo wa muendelezo wa mfumo wa kufanya kazi katika mwili kwenye kiungo chochote .
   Vidonda vya tumbo hivi viko kwenye line ya utumbo nje unoitwa "deudonum"na ndani  ya utumbo huitwa Gastric ulcers.

Vidonda vya tumbo husababishwa na acidi ikizidi tumboni,mfumo wa kumeng'enya chakula umevalishwa koti linaitwa "mucous layer" kazi yake ni kulinda acid isipite hapo.Sasa hii layer ikipungua na asidi ikizidi huleta maumivu ya kuunguza. Mfano wa kidonda kikiingia chumvi.
   Bacteria nae Helicobacteria pylori wanaishi kwenye mucuos hushambulia hii mucous na kusababisha acid kuunguza eneo hilo.

    
    Madawa ya kutuliza  maumivu. Kwa wale wanotumia dawa hizi mara kwa mara Asprin, Ibuprofen, Naproxen,Ketoprofen,n.k na ni common hutokea kwa watu wazima wanaotumia dawa zaidi,si unajua tena utuzima!!.
     OSTEOARTHITIS na OSTEOPOROSIS huu ni ugonjwa dawa zake ni Actonel,Fosamax,na potassium supliments.
  Uvutaji na unywaji wa pombe ni hatari kwa vidonda vya tumbo.

Dalili za vidonda vya tumbo.
     Maumivu ya kuunguza, hapa ndo ile pale palipoathirika panakutana na acid,kutapika damu, damu ya rangi  damu ya mzee kwenye choo kikubwa,kupungua uzito, kupoteza hamu ya kula,na uchovu uchovu kama kulegea legea hivi.
  Inashauriwa maumivu yakizidi muone daktari.

Vipimo vyake hutazamwa kwa damu,pumzi,choo kikubwa,ikishindikana inatumika  "ENDOSCOPY''.

Matibabu yake kwanza hutegemea kisababishi cha hivyo vidonda.
Yaweza kuwa dawa ya kuua bacteria,dawa ya kuzuia acid, Omeprazole,lansoprazole,rebeprazole(aciphex),pantropazole(protonix),hii hupunguza gesi tumboni pia.
Dawa ya kuzuia kuzalisha acid tumboni Histamine (H-2)blocker ambazo ni Raniticidone(zantac),famotidine(pepcid),limitidine(tagamate),nzatifine(axid).
Dawa ya kunutrolize acid ni Antacids, hii matokeo yake kusababisha kuharisha,kukosa choo.
Dawa ya kulinda upande wa tumbo ni Cycoprotective inalinda tissue tumboni.
Haziponeshi ulcers hutuliza maumivu.
 
Kinzani ulcers,(Refractory ulcers) hii ndo mbaya na haiponi ,huweza kusababisha cancer ya tumbo.
Tiba yake ni kukatwa sehemu yenye vidonda na dawa za antibiotics kwa wingi na kwa muda.
  Tunajua kwamba kutumia dawa mara kwa mara sio vizuri.

                     ILA
Lisilo budi hutendwa!!

Hivi baadhi ya vitu vya kuacha ukiwa na vidonda vya tumbo;
Usinywe dawa bila maelezo . Utumiaji wa tumbaku mara kwa mara.Uvutaji na kunywa pombe.

Vyakula vya mgonjwa wa vidonda vya tumbo

 Hakikisha unapata mlo kamili Balance diet. Matunda kwa wingi ambayo sio machachu kama embe bichi, passion.Nafaka nzima. Jizuie stress .Fanya mazoezi sana ya kujenga mwili, sio ngumi.Vyakula vyenye nyuzi yaani fiber kama Oats,nafaka,maharage makavu yalochemshwa vizuri. Vitamin 'k' inapatikana kwenye mboga za kijani, zinc inapatikana kwenye Chaza,ufuta,dark chocolate,ini za wanayama halali,karanga.

Wanaugunduzi wanathibitisha hakuna haswa chakula kinachosababisha au cha kujizuia nacho kwa ajili ya vidonda,ikifahamika kwamba ni jukumu letu kula Mlo kamili.

 Samaki wa mafuta mengi kama Dagaa,saradini,silli,salmoni,Matunda kama karoti,kale,juisi ya kabichi,kiwi fruits,apricot. Mbegu za alizeti,maharage ya soya,chammomile tea,amino acid,maziwa ya mgando yasokuwa na mafuta mengi. Hivyo ni baadhi ya vyakula vinavoshauriwa kwa mgonjwa wa vidonda ya tumbo.

Vyakula vinavoshauriwa asitumie mgonjwa wa vidonda vya tumbo ;

Vitu vya maziwa maziwa au chakula kilochanganywa na maziwa kwa wingi.Nyanya ina acid nyingi,vitunguu,vitunguu thoum,pilipili,mdalasini,vyakula vinavoongeza uzito kama ugali,vyenye wanga na mafuta tele.viungo vya chakula kwa wingi,acid kama Cola,matunda machachu,kahawa,pombe, chocolate,pickled foods, soy sauce, chumvi ya juu ya chakula sio ile ilioivia kwenye chakula,chewing gum,chakula kilopoa na cha baridi sana,nyama za mafuta,sukari nyingi, vyakula vya kukaangwa  sana.

 Inashauriwa kula mara sita kwa siku kidogo kidogo,kuliko milo mitatu ya nguvu.Usile  saa tatu 3hrs kabla ya kulala ule upumzike kidogo ulale.Baada ya kula pumzika na kutulia.

ILANI:

Tafadhali usitumie dawa mpaka ushauri wa daktari.Hakikisha unafahamu kisababishi cha vidonda vya tumbo.Kwa dalili zozote kama hapo juu nenda kwa daktari.Utumiaji wa dawa kiholela sio mzuri kwa afya yako.Unaweza kujikinga na vidonda vya tumbo.Kujikinga na maambukizi ya bacteria Hpylori anambukiza baina ya mtu na mtu.Chakula na maji pia. Unaeza zuia bacteria huyo kwa kupika vyakula viive vizuri,kuosha matunda vizuri,kunawa mikono mara wa mara na kabla na baada ya kula.Kula vizuri kabla ya kunywa dawa na kutumia maji.Usinywe pombe wakati unameza dawa.

      

0 comments:

Post a Comment