• LinkedIn
  • Join Us on Google Plus!
  • Subcribe to Our RSS Feed

Wednesday, October 30, 2013

ASALI (chakula cha afya duniani).

1:38 AM // by Kalma // No comments

ASALINi ya ajabu yenye rangi ya dhahabu.Hupatikana ndani ya mwaka mzima kila siku.

 Ni chakula kitamu cha nyuki hutumia nectar kutokea kwenye maua.Aina ya Apis ndo hujulikana zaidi.Hukusanywa na wafuga nyuki,na hutumika sana kwa binaadamu.

 Asali inayotengenezwa na wadudu wengine hiyo ina matumizi tofauti. 

Nyuki wanatengeneza asali kwa njia ya uchavushaji(regurgitation)na uvukizi(evaporation).wanaihifadhi katika mizinga ya nyuki.

Ni tamu hulinganishwa na sukari tena huzidi hata hiyo sukari yenyewe.Bacteria wengine hawazaliwi kwenye asali sababu ya maji yako 0.6, kuna bacteria Clostridium Botulimum nae ni hatari kwa watoto wachanga.Ina madhara kwa ukuaji wa Intestinal tracts,hupelekea kuumwa sana hata kifo wakati mwingine.

Asali ina historia kwa binaadamu hutumika kwa vyakula na vinywaji,kuongezea ladha na utamu.Huaminika kidini.

Asali ni dawa.Asali ziko tofauti kulingana na grade na chanzo cha  nectar iliopatikania na maua pia.Ina sukari ya asili dehydrated ambayo hukinga na fermentation.

Hutengenezwa na nyuki kama chakula cha kwao wenyewe sana sana kipindi cha baridi kali na kipindi chakula fresh kikipungua maana yake maua na vyanzo vingine vya vyakula vyao hao nyuki,au hakipatikani,nyuki hutumia asali kama chanzo cha nguvu.


Kuna nyuki wanawake ambao ni Queen,kuna nyuki wanaume,na kuna wanaume wa msimu hawa ni kwa ajili ya fertilization kwa Queen wapya. Wanawake ndo wachapakazi 20,000-40,000.
 Muonekano wa asali unatofauti hutegemeana na maji yalokuwemo,na aina ya flora ilotumika kutengenezea,hali ya hewa,na portion ya sukari iliokuwemo.
Fresh honey ina liquid,maji, sukari nyingi na maji huyeyuka kutegemea hali ya hewa iliopo.Ina Fructose na Glucose.
Egypt wanatumia asali kwa kuongeza ladha ya cake na biskuti, na vyakula vyao vingi hupendelea kutoelea asali .

        Asali imetajwa kwenye uislam sana katika Qur-an na kuna surah inaitwa An-Nahl(the bee).Na ipo Hadith ya Mtume Muhammad(S.A.W) amesema Asali hutuliza maumivu ya magonjwa.
Na Qur-an inasisitiza asali ni kirutubisho cha chakula chenye afya. Qur-an(16:68-69)Jewish wao asali kama ishara ya mwaka mpya na huliwa zaidi siku hiyo,wanakula kwa kuzamisha apples kwenye asali na kuutakia mwaka kuwa mtamu . Asali hupikiwa,hutumika kuokea,kupakaa kwenye mkate na nyongeza kwenye vinywaji. Kama chai, vilevi kama honey wine,or honey beer.

Asali ina mchanganyiko wa sukari na vingi virutubisho.Ina Carbohydrates,Fructose(38.5%),Glucose(31.0%).Asali hubaki na Carbohydrates  yenye Maltose na Sucrose na madini pia.Achilia utamu wake ina Vitamin na madini ya kutosha.
Ina fanya kazi ya Antioxidants, ikiwemo Chysin,Pinobanksin,Vitamin C,Catalase na Pinocembrin. Hutegemea na mmea ulozalisha asali yenyewe.


   Kuna asali ya maua na ya kutengenezwa,bali zote hutokea kwa maua.
Asali ni kitu pekee chakula cha afya na dawa pia,asali huweza kihifadhiwa kwa muda wa mwaka na hata karne, kwa kutegemeana na humidity iliyopo.

          Hutibu magonjwa
Gastric inayopelekea ulcers.Vidonda na kuungua.Antiseptic na antibacterial.MRSA infections.Kulainisha koo na kutuliza kikohozi.Hutoa rushes .Huondoa na kupunguza allergies.Hupunguza high cholesterol.

Mtoto chini ya mwaka haishauriwi kupewa asali sababu ya Botulism iliopo huweza leta madhara katika mfumo wa  digestion. Asali ina sumu endapo italiwa kabla haijatengenezwa inasababisha Kizunguzungu,uchovu,kutapika na nausea.Pia kwa mbali huweza sababisha presha,shock na mapigo ya moyo yasiyo kawaida sio sana nayo hii kutokea,very rare.Sumu hupatikana sana msitu Tutu kwa vine Happer insect huko Newzealand.Sumu yao inaitwa Tutin ipo kwenye asali. Ni kutokula hii aina ya asali na dalili zake ni kutapika,kuweweseka,kizunguzungu,coma n.k.

   
Nchi inayoongoza kuvuna asali ni China,Uturuki na Ukraine.Tanzania Tabora wanashika namba kwa kuvuna asali wakifuatiwa na wengine Singida,kigoma,n.k.
   
Tips ya kuiandaa asali na kupikia.

Kama asali yako imeganda.chukua chombo tia maji moto na kisha weka asali yako kwa dakika 15 itayeyuka.Usiipashe asali kwenye microwave.Tumia asali ikiwa kama kimiminika .Huwa nzuri ikiwekwa badala ya sukari.Katika kupikia tumia 25F sababu asali mara moja kufanya chakula kibadili rangi kuwa brown na hata kuungua.

      FURAHIA ASALI .

Tumia asali mezani kama sukari kwa chai. Chovyea apple kwenye asali.Weka kwenye maziwa ya mgando kama sukari.Sandwich nzuri inayopendwa na watoto ni ile yenye Peanut butter,ndizi na asali."MILK DRINK" Chemshia maziwa ya soya,asali na dark chocolate ambayo sio tamu,kwa moto mdogo.

Urembo wa asili wa uso na ngozi huwezi ukaiacha asali,hutumika kwa kupakaa usoni na hata kujisugulia mwilini.Chukua pumba laini changanya na asali msugulie bi harusi mtarajiwa kwa muda wa wiki nzima mara moja hata mbili,afanye waxing na apakae hinna.



0 comments:

Post a Comment