Wanaume hupendelea kupakaa kwenye nywele na ndevu hii iko sana kwa wasomali kwenye nywele .
Na wazee kuondoa ile rangi ya mvi kwenye nywele.
Henna ya kwenye nywele inaweza changanywa na Cassia Obovata kwa kuleta blond color, mafuta na waxes na metal salts ikichanganywa na chemical treatments.
Huchanganywa na maji moto pia.Henna hutumika sana kwa urembo haswaa wa kujipakaa kwa sherehe tofauti tofauti,japo mwanzoni ilionekana kwa bi harusi zaidi na fetility celebrations.
Ilianza kwa Baal na Anath kwa sherehe ya kupokea waume zao.
India wanaamini Henna aloipaka bi harusi ikichelewa kutoka huashiria ndoa ya furaha na kupendwa na in-laws, na ikiwahi kutoka maana yake ndoa haitakua na furaha.
Ukaona sababu ya kuikoleza henna ikolee sana ili isitoke haraka.
Saudia Arabia wao kule bi harusi anapakaliwa henna na ndugu yake wa karibu mwenye ndoa ya furaha la si hivyo atamletea ishara mbaya ya ndoa.
Somalia henna huvaliwa na wanawake mikononi kipindi cha harusi,Eid,Ramadhani n.k.
Tunisia wanasherehekea henna kwa siku saba .Siku ya tatu bi harusi anavaa nguo za mila huku akipakaliwa henna mikononi na miguuni. Kwa mwanaume bwana harusi anapakaa pinky finger siku ya sita.
Tanzania kote hutumika kwa urembo wa bi harusi, nywele,Eid, na kupakaa kwa aliyeolewa kama urembo kwa mume wake na sana sana pande za pwani.kwa wale ambao bado kuolewa hupakaa kidogo tu tena siku maalum, kama sherehe n.k.
Henna hutumika kuondoa kuungua kwa ngozi ilosababishwa na jua na athletes foot.
Henna hutumika kwa tatoo na iko salama sababu hutumika henna ya asili ile ya majani.
Majani ya henna yanatumika kutengenezea henna ambayo ni dawa ya kuzuia kuharisha kunakotokana na parasites(ameoba),cancer ,kupanuka kwa wengu(enlarged spleen),maumivu ya kichwa,homa za manjano,na ngozi.
Siku hizi hutibu tumbo na maradhi ya ulcers.
Henna hupunguza m-ba kwenye nywele,eczema,mapele,fangasi,na vidonda.
Hutumika kwa kunywa ilo chemshwa na kupakaa ilochemshwa pia.
Henna ina madhara kutokana na dawa wanazochanganyia siku hizi kama kuvimba na kuungua mfano wa malengelenge.
Kama henna ya tatoo hutumika black henna hii huwekwa PPD ambayo ina kama mfano wa lami ambayo haiko salama kwa ngozi.
Huleta madhara kama vipele kwa ngozi,kuunguza,makovu,blistering,n.k.
Ni vizuri kutumia henna ya asili yaani ya majani kuepusha hizo rubsha zote.
JINSI YA KUPAKAA HENNA KICHWANI.
Kupakaa henna sio kama kupakaa rangi nyingine za nywele au kushika pizza sauce na meat balls.Nywele zikiwa refu na kazi huwa ngumu kidogo ila hupendezesha nywele sana.
Pakaa vaseline sehemu za usoni karibu na nywele.husaidia kutopata doa vya rangi.Unaweza kupakaa henna kwa nywele kavu au zilolowa ila nzuri zaidi kwa nywele kavu.
Vaa taulo shingoni au nguo mbaya mbaya. Vaa gloves kisha kata mistari mapande manne ya nywele.Pakaa henna kuanzia chini yaani kwenye ngozi nakupanda juu.Anzia fungu la nyuma na huwa rahisi .Ziache kwa saa 2-4,ukizidisha muda nayo hukolea zaidiKulala nayo usiku kucha ni nzuri ukiwa umevaa kofia ili usichafue shuka.Osha vizuri kwa shampoo unayotumia. Hakikisha henna imeisha vizuri kwenye nywele.
Ya kuzingatia;Pangusa haraka endapo imedondokea kwa ngozi tumia maji na vaseline .Osha conditioner badala ya shampoo.Henna hukolea zaidi siku za mbele. Hudumu kwa muda wa mwezi na kuendelea.Changanya Indigo baada ya kupakaa henna kwa brown color.Pakaa mafuta muda wa usiku tumia Mastard oil ni mazuri kwa kukolezea rangi ya hennaTumia henna baada ya miezi sita kama ulitumia chemicals kwa nywele zako mfano relaxer,au rangi nyingine.Henna hutumika kama dhahabu kwa wale ambao hawana uwezo wa kuvaa dhahabu mikononi.
0 comments:
Post a Comment