KUOSHA VYOMBOKuosha vyombo,vijiko,uma, visu cutlery ni sheria baada ya kula mlo wa chakula huwa vimechafuka na kwa sababu za kuua vijidudu na magonjwa.
Tumezoea kuosha kwa mkono la sivyo dishwasher .
Vyombo vitakate huhitaji vitu vitatu;Maji, Sabuni,Osheo.Vaa gloves ni option unaweza usivae.kama mikono yako mikavu hii gloves husaidia na madhara ya ngozi kwa sabuni kali.kunja nguo au shati ya mikono mirefu. Vaa aproni ni vizuri pia.Ondoa masalio ya vyakula katika vyombo tupia kwenye hifadhio la taka,kuliko kutoa kwa kutumia sponji ya kuoshea . Tumia maji moto kama inawezekana.Maji moto yanakata mafuta na huua vijidudu,na hutumika kidogo na hutoa sabuni haraka.Na kwa wanaotumia maji ya chumvi kama ya visima ndio bora zaidi. Anza na vyombo vya silver kama uma,vijiko,visu, sababu vinatumika zaidi mdomoni huhitaji usafi wa hali ya juu.Osha vingine vinoshikwa pia mdomoni yaani glass,vikombe tumia maji moto.Osha pots na sufuria ambavyo ni vichafu zaidi kwa maji mengi.loweka kwanza kama kuna vilivogandia au mafuta ongeza sabuni kwa kusugua na uviache ukiwa umeloweka na maji,huku endelea kuosha vingine,navyo ni sahani na bakuli za kupakulia. Weka vyombo katika reki vijichuje,halafu unaweza kukausha kwa kitambaa kikavu.
Tembeza mkono katika vyombo kuhakiki vimetoka mafuta,kama vidole vitateleza huashiria mafuta hayajaisha na urudie kuosha tena.Osha brush na viosheo vyote,viache vikauke.Ili visitoe harufu sababu harufu haiondolewi kwa kusuuzwa tu.
Unaweza tumia steelwool kwa kusugulia masufuria au mchanga wa baharini laini ni mzuri kwa kung'arisha na kuua vijidudu,na sufuria hazichakai haraka.
TIPS;Ukitaka kutumia chombo baada ya kukiosha,tumia kitambaa aina ya linen kukaushia,hii haiachi nyuzi nyuzi.Osha kila mahala pa chombo.haswa vyenye urembo na mshikio wa vijiko pia.
Loweka mara tu baada ya kupikia kwa vile vilivogandia.Viosheo vya sponji au nguo ni nzuri kwa kuondoa mafuta .Kama unatumia kiosheo kuondolea mauchafu ya vyakula osha vizuri kabla hujatumia tena kuoshea vyombo.
Vinegar,ndimu pia,nzuri kusuuzia vyombo huondoa harufu,huua vijidudu,na hung'arisha vyombo.
Usiweke kisu kwenye maji ya vyombo uloloweka na sabuni,huweza kukukata pindi unapokitafuta .
Sponji,nguo,brush hushika bacteria kwa urahisi,kupunguza bacteria kwa vitu hivyo ni kuloweka na kuvikausha . Ni vizuri kufua vitambaa kwa maji moto hata kuvichemsha kwa dk kumi(10)na lowekea dawa.
Pakaa mafuta nje ya sufuria endapo utapikia kuni au mkaa utaosababisha masizi,ni rahisi kusafisha, na gharama ndogo. Hii unaweza tumia kwa vyombo vya kuokea kama mkate,cake,buns,kashata n.k hurahisisha wakati wa kutoa chakula wakati wa kukipakua.
0 comments:
Post a Comment