JINSI YA KUOSHA USO
Kuosha uso ni kazi rahisi sana na kitu muhimu kwa ngozi yako na muonekano mzuri wa kuvutia.
Kama hujui jinsi ya kuosha uso fuatilia hii;
Rudisha nywele zako nyuma kwa wale wenye nazo,unaweza tumia kibanio kuzibana hata rasta namaanisha,au kofia,ili kupata ngozi ya uso tu.
Mwagia maji ya uvuguvugu uso mzima.unaweza kuacha yakikumwagikia tokea shower,maji ya uvuguvugu yanafungua vinywelea(pores), vya usoni na uso husafishika vizuri.Epuka kutumia maji baridi ikiwezekana,acha uso kwa dakika chache kwenye maji ya uvuguvugu.
Pakaa sabuni kwa kuzunguka uso.sugua taratibu,ukitumia nguvu waeza chubuka.Huhitaji aina nyingi za sabuni.
Tumia kitambaa laini kujisugua ukitumia facial scrub. Inasaidia kutoa uchafu kwenye ngozi na kufungua pores.
Suuza na maji kutoa sabuni.Tumia mkono,rudia mpaka sabuni ziishe kabisa.kama sabuni hazitoki lowanisha kitambaa laini na safi futia kwacho.
Tumia kitambaa laini kusafishia uso.
Pakaa toner kwa kutumia pamba tumia ambayo haina kilevi.
Pakaa mafuta laini (moisturizer) husaidia kuweka uso wenye afya,na kung'aa vizuri.
Kama unatoka tumia kilainishi chenye kuzuia jua,"sunscreen" SPF 15 or 30.
TIPS
Hakiki mikono yaako misafi kabla ya kuosha uso .Fanya taratibu usitumie nguvu.Osha uso mara mbili kwa siku.Epuka kutumia taulo kwa uso na mwili .Osha uso kwa maji ya uvuguvugu,before toning, halafu suuza kwa maji baridi haraka kwa mara moja,maji moto yatafungua vinywelea vyenye mafuta yalozidi,na maji yaliyopoa sio ya moto sio ya baridi sio ya uvuguvugu,yatafunga vinywelea.Tumia product inayofaa kwa ngozi ya uso wako.Pendelea kuosha uso baada ya kuoga.Tumia mafuta kukandia uso kwa muonekano mzuri na afya. ILANI
Usilale na make-up usoni.Kama una ngozi sensitive, weka kitone kidogo kwenye mkono kwa dakika kumi kwa kuangalia reaction yeyote.Usioshe saana uso.Usitumie kitambaa mara mbili bila kukifua.Usitumie maji moto yataunguza uso.
"A clean face is a beautiful face"
Tunashkur kwa facial wash ideas but I have one concern.. Umesema tuepuke maji baridi kisha huku chini umeonesha umuhim wa maji baridi... And kwa kuongezea it's advised tusioshe USO Na sabuni kwakua sabuni ina toa acidity iliyoko Usoni hivyo kuwafanya bacteria waweze kuzaliana kwa urahis. Kwa kawaida USO unatakiwa uwe balanced so OSHA USO na facial wash isiyo Na sabuni, hua zinaandikwa 'no soap' kisha baada yakuosha Na maji ya uvuguvugu Tia maji ya baridi ili kufunga vitundu vilivyoko Usoni. Bila kusahau kunywa maji mengi, matunda Na mboga mboga ili kutengenexa ngozi nyororo Na yenye afya... Asante my wii
ReplyDelete